Rwanda inasema itawaruhusu Waafrika kuingia bila visa nchini humo.
"Mwafrika yeyote, anaweza kupanda ndege kwenda Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu," alisema rais Paul Kagame wakati wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Utalii Duniani.
Rais Paul Kagame alitoa tangazo hilo siku ya Alhamisi katika mji mkuu, Kigali, ambako alitaja uwezo wa Afrika kama, "kivutio cha utalii cha umoja" kwa bara ambalo bado linategemea 60% ya watalii wake kutoka nje ya Afrika, kulingana na data kutoka Tume ya Uchumi ya Afrika ya Umoja wa Mataifa.
"Hatupaswi kupoteza mwelekeo wa soko letu la bara," alisema na kuongeza, "Waafrika ni mustakabali wa utalii wa kimataifa huku tabaka letu la kati likiendelea kukua kwa kasi katika miongo ijayo."
Afrika yaanza kufungua mipaka yake
Mara baada ya agizo hilo kutekelezwa, Rwanda itakuwa nchi ya nne ya Afrika kuondoa vikwazo vya usafiri kwa Waafrika.
Mataifa mengine ambayo yameondoa viza kwa raia wa Afrika ni Gambia, Benin na Ushelisheli.
Rais wa Kenya William Ruto alitangaza Jumatatu mipango ya kuruhusu Waafrika wote kusafiri katika taifa hilo la Afrika Mashariki bila viza ifikapo Desemba 31.
"Vizuizi vya viza miongoni mwetu vinafanya kazi dhidi yetu. Wakati watu hawawezi kusafiri, wafanyabiashara hawawezi kusafiri, wafanyabiashara hawawezi kusafiri sote tunakuwa washindi,” alisema Ruto kwenye mkutano wa kimataifa huko Congo Brazzaville.
Umuhimu wa uhuru wa usafiri
Umoja wa Afrika, AU mwaka 2016 ulizindua mfumo wa kusafiri ya Afrika , ikisema utashindana na mtindo wa Umoja wa Ulaya katika, "kufungua uwezo wa bara hilo."
Hati za kusafiria za kiafrika na uhamaji huru wa watu "unalenga kuondoa vikwazo vya kusafiri kwa Waafrika, kufanya kazi na kuishi ndani ya bara lao," AU inasema kwenye tovuti yake.
Hata hivyo, ni wanadiplomasia na maafisa wa AU pekee ndio wamepewa hati ya kusafiria yeny hadhi ya kidiplomasia.
AU pia ilizindua Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, eneo la biashara huria katika bara zima linalokadiriwa kuwa na thamani ya dola trilioni 3.4, ambalo linalenga kuunda soko moja la umoja kwa watu bilioni 1.3 wa bara hilo na kukuza maendeleo ya kiuchumi.