Mauzo ya mbogamboga na matunda yaongezeka nchini Rwanda./Picha: Wengine

Mauzo ya bidhaa za mbogamboga nchini Rwanda yameongezeka kwa asilimia 29.1 na kufikia gharama ya Dola Milioni 75 kwa kipindi cha 2023/2024.

Hili ni ongezeko la kutoka Dola Milioni 58.16 kwa mwaka wa awali, kulingana na takwimu iliyotolea na Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Wanyama siku ya Januari 6.

Kulingana na takwimu hizo, mapato ya mazao ya mbogamboga yameongezeka kwa asilimia 22, wakati yale ya matunda yamekuwa kwa asilimia 61.

Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, bidhaa za mbogamboga zimechangia zaidi ya Dola Milioni 42.3, iliyotokana na mauzo tya tani 62,000 za bidhaa hizo.

Kulingana na takwimu hizo, kufanya vizuri kwa sekta ya kilimo nchini Rwanda kumetokana na ongezeko la mahitaji bidhaa za mbogamboga na matunda.

Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa, mauzo mengi ya bidhaa hizo zilifanyika nchini DRC, ikifuatiwa na Uingereza, Ufaransa na maeneo mengine ulimwenguni.

TRT Afrika