Robinho alipatakana na hatia ya kubakwa mwaka 2017./Picha: Reuters

Mahakimu wa Brazil wameshikilia msimamo wa hukumu dhidi ya nyota wa zamani wa AC Milani na Brazil, aliyekuwa anakabiliwa na shitaka la ubakaji, na kuongeza kuwa ni lazima Robinho atumikie kifungo cha miaka tisa jela nchini Brazil.

Mahakama ya juu ya Brazil (STJ), inayoshughulikia mambo yasihusu katiba, yalihalalisha uamuzi wa mahakama ya Italia dhidi ya nyota huyo, nchini Brazil.

Mwaka 2017, Mahakama ya mjini Milan ilimtia Robinho na wenzake watano hatiani kwa kumbaka mwanamke baada ya kumuhadaa kwa vilevi, ndani ya klabu ya usiku, mwaka 2013.

Hukumu hiyo ilithibitishwa na mahakama ya rufaa mwaka wa 2020 na kuthibitishwa na Mahakama ya Juu ya Italia mwaka wa 2022.

Robinho kujisalimisha

Mara zote, nyota huyo wa zamani mwenye miaka 40, amekana mashtaka hayo.

Brazil haina utaratibu wa kusafirisha raia wake na hivyo, mwaka jana Italia ikaiomba Brazil, Robson de Souza kutumikia kifungo hicho nchini mwake.

Akizungumza baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, Wakili wa Robinho, Jose Eduardo Alckmin alisema kuwa nyota huyo atajisalimisha katika mahakama pindi atakapojulishwa kuhusu maamuzi hayo.

'Hukumu bila haki'

Mahakama ya Brazil haikuwa tayari kwa majadiliano kuhusu hukumu ya ubakaji, na kuamua kuona kama uhalali wa hukumu hiyo nchini humo.

Hata hivyo, katika mahojiano yake ya jumapili na kituo kimoja cha televisheni nchini Brazil, Robinho alisema angetamani kuona kama mahakama ya Brazil itazingatia maamuzi ya Italia.

"Nilihukumiwa visivyo halali nchini Italia kwa kitu ambacho hakikufanyika," amesema.

TRT Afrika