Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekabidhi madaraka kwa makamu wake wawili kwa kipindi cha mwezi mmoja wa likizo yake ya kila mwaka iliyoanza Disemba 31, 2024.
Rais atatumia likizo yake nchini hadi atakaporejea ofisini mwezi Februari, gazeti la serikali la Herald lilimnukuu Katibu huyo wa Baraza la Mawaziri.
"Rais atapatikana kwa ahadi zinazohitaji uangalizi wake binafsi, kama rais wa nchi na kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)," alisema George Charamba, Katibu wa Baraza la Mawaziri.
Makamu wa Rais Kembo Mohadi na Constantino Chiwenga watachukua nafasi yake kwa zamu.
"Makamu wa Rais Mohadi atachukua hatua kuanzia Desemba 31, 2024 hadi Januari 19, 2025. Baada ya hapo, Makamu wa Rais Chimwenga atachukua uongozi hadi rais atakaporejea kazini," Charamba alisema.
Rais Mnangagwa, kiongozi wa Zimbabwe tangu 2017, ametaka kushirikisha serikali za Magharibi kurejesha uhusiano, kutatua deni kubwa la nje la Zimbabwe na kufufua uchumi wake.