Samia

Kupitia taarifa kutoka Ikulu iloyoeleza kuwa Rais Samia ametoa tamko hilo leo wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya miaka 60 ya mkoa huo yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadia.

Aidha, Rais Samia amewataka viongozi kuwahamasisha wananchi kupanda mazao yanayostahamili ukame pamoja na kutumia mbegu bora na za muda mfupi.

Rais Samia pia amewahimiza wananchi kulima mazao ya alizeti, dengu na ufuta ambayo hustawi katika maeneo mengi ya mkoa wa Singida pamoja na zao la korosho ambalo pia linafanya vizuri katika maeneo mengi ya mkoa huo.

Vile vile, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha miradi ya umwagiliaji inatekelezwa katika maeneo yote yaliyobainishwa kwa ajili ya ujenzi wa skimu.

Awali Rais Samia alizindua daraja la Msingi lenye urefu wa mita 100 lililopo Wilaya ya Mkalama ambalo limegharimu kiasi cha takribani shilingi bilioni 11.2.

Akihutubia wananchi wa Mkalama Rais Samia amesema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto za kisekta zinazoikabili wilaya hiyo hususan elimu, afya na maji.

TRT Afrika