Rais Putin hatahudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini

Rais Putin hatahudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini

Viongozi wa BRICS watafanya mkutano wao wa 15 nchini Afrika Kusini mwaka huu
Afrika Kusni imesema kuwa Urusi haitahudhuria mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini / Picha: AP

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha Afrika Kusini inasema kuwa rais wa Urusi Vladmir Putin hatahudhuria mkutano wa muungano wa BRICS ambao umepangwa kufanyika Afrika Kusini mwaka huu.

Brazil , Urusi, India na China zilifanya mkutano wao wa kwanza mnamo 2009 nchini Urusi kabla ya Afrika Kusini kujiunga mwaka 2010.

Nchi za BRICS zimekuwa injini kuu za ukuaji wa uchumi duniani kwa miaka mingi.

"Kwa makubaliano ya pande zote rais Vladimir Putin wa Shirikisho la Urusi hatahudhuria mkutano wa marais lakini shirikisho la Urusi litawakilishwa na waziri wa mambo ya nje Sergey Lavrov," msemaji wa rais Vincent Magwenya amesema katika taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari .

"Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa Brazil India China na Afrika Kusini," ameongeza.

Mkutano wa viongozi wa BRICS utafanyika kwa mara ya kwanza tangu janga la Uviko-19 na vikwazo vingine vya dunia.

Kumekuwa na majadiliano kimataifa kuhusu kukamatwa kwa rais Putin akikanyaga nchini Afrika Kusini. Hii ni kwa sababu Afrika Kusini ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na inatarajiwa kumakata Putin akifika huko.

Afrika Kusini imekataa kuegemea upande wowote katika mzozo kati ya Ukraine na Urusi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliongoza ujumbe wa amani wa viongozi wa Afrika, Juni kwenda Ukraine na Urusi wakiomba nchi hizo mbili kuacha vita.

TRT Afrika