Rais Mnangagwa wa Zimbabwe aapishwa baada ya kura ya maoni yenye utata  

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliapishwa Jumatatu kwa muhula wa pili baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi uliopita uliokumbwa na utata, huku akiahidi kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka katika umaskini.

Raia wa Zimbabwe walipiga kura Agosti 23 kumchagua rais mpya, wabunge na wajumbe wa baraza la mitaa, lakini chama kikuu cha upinzani kilielezea matokeo hayo kama "udanganyifu mkubwa".

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Mnangagwa aliomba umoja baada ya uchaguzi, akiahidi kufufua uchumi unaodorora.

"Sera sikivu ambazo zilianza katika muhula wangu wa kwanza kama rais ziko njiani kuwaondoa wengi kutoka kwa umaskini," Mnangagwa alisema.

Maelfu ya wafuasi wa Mnangagwa, wengi wao waliingia kwa mabasi kutoka kote nchini, waliimba na kucheza wakati mzee huyo wa miaka 80 akiingia kwenye Uwanja wa Michezo wa Kitaifa pamoja na mkewe.

Reuters