Na Abdulwasiu Hassan
Malori yaliyosheheni nafaka yanatoroka nje ya Nigeria kupitia njia zisizo rasmi huku raia wakikabiliana na changamoto ya mfumuko wa bei.
Ukubwa wa tatizo hilo unaakisiwa na kauli ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo Kashim Shettima ya kukubalina na tatizo hili, katika mkutano wa usimamizi wa mali uliofanyika Abuja mnamo Februari 20.
"Ni hivi majuzi tu, malori 45 yaliyosheheni mahindi yalikamatwa yakiwa yanaelekea nch jirani," Shettima aliambia hadhira hiyo. "Baada ya kukamatwa kwa shehena hiyo, bei ya mahindi ilishuka kwa N10,000...Kuna sababu ambazo zinalenga kuhujumu taifa letu."
Kabla ya hutoba, idara za forodha za nchi hiyo zilitangaza matukio ya kukamata malori ya mizigo ikiwa inatoroshwa nje ya nchi hiyo kupitia njia tofauti zikiwemo za jimbo la Jigawa State, linalopatikana kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Idara za forodha nchini Nigeria haziwi sehemu ya habari kuu kuhusu udhibiti wa utoroshwaji wa bidhaa za chakula nje ya mipaka ya nchi hiyo. Bali katika jukumu lake la uingizwaji wa bidhaa za chakula kama vile mchele katika kufanikisha sera za serikali za uingizwaji wa bidhaa.
Miaka michache iiliyopita, Nigeria ilikuwa inakabiliana na changamoto kubwa ya kudhibiti magenge na mitandao ya uturoshwaji wa mafuta yenye ruzuku nchi jirani.
Baada ya mamlaka kushindwa kudhibiti hali hiyo, waliamua kufunga mpaka wa nchi na Benin, kwa upande wa Seme, mwaka 2019. Hatua hii ililenga kuwalinda wakulima na wakoboaji wa bidhaa za mpunga wa bei rahisi kutoka jamhuri ya Benin.
Kwa mujibu wa serikali, hizi ni kati ya sababu za kuondoa ruzuku ya mafuta ili kuepuka matatizo zaidi.
Kwa sasa, Nigeria inapitia hali mbaya ya mfumuko wa bei, ambao umefikia asilimia 35.41, kulingana na ofisi ya takwimu ya nchi hiyo.
Nchi hiyo inachukua hatua kali za kupunguza mfumuko wa bei katika bidhaa za chakula, japo bado safari ni ndefu.
Hatua za mageuzi
Nigeria imetoka kwenye kuweka utegemezi kwenye naira ili pesa hiyo ipate thamani yake halisi. Hatua hii, pamoja na kuondoa ruzuku kwenye mafuta ni sehemu ya mageuzi na maboresho yaliyotangazwa na Rais Bola Ahmed Tinubu alipoingia madarakani mwezi Mei.
Hali hii ilipelekea kuporomoka kwa sarafu hiyo kutoka 450 kufikia dola moja hadi 1,500 katika soko la kubadilishia fedha.
Kushuka kwa thamani ya sarafu ya Nigeria kulitokana na mabadiliko ya sera, faranga ya CFA ya Afrika Magharibi na faranga ya CFA ya Afrika ya Kati zinazotumiwa na majirani wa Nigeria ambazo, zimezipiku kwa sasa.
Hali hii imeongeza gharama uingizwaji wa chakula kutoka Nigeria.
Wataalamu wanasema kuwa hii ni moja ya sababu inayosababisha malori mengi ya shehena za chakula kukamatwa na idara za forodha za nchi hiyo.
Hasara kubwa
Ingawa njia hiyo inaonekana kufanya kazi, kwa upande mwingine inaongeza gharama za maisha kwa raia wa nchi hiyo.
Rais Tinubu amekiri kwama baadhi ya mageuzi hayo yameleta maumivu kwa wananchi wa kawaida wa Nigeria, lakini akasema yatakuwa ni ya muda mfupi.
Pia aliagiza kutolewa kwa nafaka kutoka maghala ya serikali kama sehemu ya kudhibiti mfumuko huo.
Idara za forodha zimeanza kuuza magunia ya michele iliyokamatwa kwa bei ya kutupa, ya kuanzia N10,000 kwa gunia la kilo 25.
Vipenyo mipakani
Makamu wa Rais Shettima alisema kuwa njia zisizo rasmi ziligunduliwa katika eneo la Illela, kwenye jimbo la Sokoto.
Ukubwa wa tatizo hilo unapimwa kutokana na uhalisia kwamba mpaka wa Illela ni sehemu ndogo tu ya mpaka wenye kilomita 1,600, unaotenganisha Nigeria na Niger. Nchi hiyo pia inapakana na Chad na Cameroon.
Inakadiriwa kuwa kuna njia zisizo rasmi zaidi ya 1,000 na hivyo kuwa ngumu kuzuia mianya hiyo.
Hoja za kinadharia zipo kwa biashara iliyowekewa vikwazo, ingawa hilo na chaguo la kufungwa kwa mpaka hufanya sera ya kiuchumi ya kizamani katika ulimwengu wa kisasa, uliounganishwa.
Kuna zaidi ya kupata ikiwa nchi itashiriki katika makubaliano ya kimkakati ya biashara huria. Kutofungua kwa ushindani kunaweka viwanda vya ndani vikiwa duni na visivyofaa, huku gharama kubwa ya uzalishaji ikidhoofisha ustawi wa jumla wa watu.
Nigeria inaweza uwezekano wa kupunguza bei ya chakula kwa kuongeza usambazaji kupitia biashara ya kimkakati, kubadilisha sera za kiuchumi zinazoongeza gharama ya uzalishaji na, kwa muda mrefu, kuwekeza sana katika kilimo na kufungua sekta hiyo kwa uwekezaji wa kimkakati wa kigeni wa moja kwa moja.
Udhibiti kwenye soko la fedha la nje ni njia nyingine ifaayo.
Kampeni ya pamoja
Baada ya taasisi ya kuzuia rushwa ya kaskazini magharibi mwa jimbo la Kano kuanza kuwalenga wanaohusika na kuhodhi chakula, Rais Tinubu aliwataka maofisa wa ulinzi wanaendeleza tabia hiyo katika sehemu tofauti za nchi hiyo.
"Huo ni wakati wetu kuwa kitu kimoja, tumuunge mkono Rais wetu, serikali yetu. Tunazo rasilimali, tunao uwezo wa kubadilisha hali ya mambo. Tunaelekea kuimarisha uchumi wetu," alisema Babajide Sanwo-Olu, Gavana wa jimbo la Lagos.
Aliongeza kuwa serikali katika jimbo lake, ilikuwa inahamasisha ukulima wa mijini, kama hatua za mwanzo.
"Ni wakati muafaka kuanza kula kile tulichopanda na kuwa kile tunachokula. Tuendelee kupanda chakula zaidi," Sanwo-Olu aliwaambia raia wa jimbo lake.