Muonekano wa mbele wa treni ya kisasa ya SGR ya nchini Tanzania./Picha: TRC

Safari za reli ya kisasa ya SGR nchini Tanzania zilitatizika kwa muda kufuatia hitilafu ya umeme katika miundombinu ya reli hiyo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli la nchini Tanzania (TRC), hitilafu hiyo ilijitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha treni hiyo ya kiwango cha kimataifa (SGR) kusimama kwa muda wa saa mbili.

Tukio hilo linakuja siku moja kabla Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan kuzindua safari kuzindua treni ya kisasa.

Hata hivyo, mafundi wa shirika hilo walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme huo, hatua iliyowezesha treni hiyo kuendelea na safari yake.

TRT Afrika