Na Gokhan Batu
Ushindi wa hivi karibuni wa Donald Trump kama Rais wa Marekani hautarajiwi kubadilisha uungaji wake mkono kwa Israeli. Hata hivyo, uhusiano wake na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu hautegemewi kuwa sawia kama ilivyokuwa wakati wa muhula wake wa kwanza madarakani.
Netanyahu amekabiliana na changamoto za kutosha wakati wa utawala wa Biden kuanzia mwezi Januari 2023.
Hata hivyo, kwa kuzingatia aina ya uongozi wa Trump wakati wa muhula wa kwanza, kuna hoja kuwa inaweza kuwa vigumu kwa Netanyahu kuendelea na kasi ile ile. Uhusiano wa viongozi hao wawili pia ni hoja ya msingi kwa sasam kwani wakati Trump akipinga matokeo ya Urais wa 2020, Netanyahu alikuwa akimpongeza Biden kupitia picha mjongeo, huku Trump akiiita ishara hiyo kuwa ni dharau.
Nguvu ya Trump, ujasiri wa Netanyahu
Baada ya michakato mitano ya uchaguzi toka mwaka 2018 na kipindi cha changamoto za kisiasa, Netanyahu alirudi madarakani mwishoni mwa mwaka 2022 kwa kukiunga mkono kikundi cha kisayuni kuingia bungeni. Hata hivyo, hatua hiyo bado inamuweka mashakani hasa ukizangatia uvamizi wa Oktoba 7.
Netanyahu amekua msikivu zaidi kwa matakwa ya washirika wake wa muungano, ambao mwendelezo wa serikali yake unategemea, na wakati mwingine amejitahidi kudhibiti mpasuko ndani ya chama cha Likud.
Kutokana na hali hiyo, Netanyahu kwa sasa anashikilia nafasi ya kiongozi ambaye ameweza kubakia madarakani kupitia mbinu mbalimbali. Akikabiliana na changamoto nyingi za ndani, anafahamu kuwa mwaka wa 2025 unapokaribia, shinikizo la uchaguzi litaongezeka, na kwamba, licha ya kucheleweshwa, uchunguzi tukio la Oktoba 7 bado hauepukiki. Zaidi ya hayo, wimbi la wanaharakati wa upinzani ambalo lilianza na maandamano mwaka 2023 limeendeleza azma yao huku likilenga kubadilika na kuwa vuguvugu la nguvu linalolenga uokoaji wa mateka baada ya uvamizi wa Oktoba 7.
Ufinyu wa uchaguzi wa sera za kigeni
Michakato ya uchaguzi wa Israeli umekosa kipengele cha sera a kigeni toka miaka ya 2010. Kipindi hicho, Netanyahu alikuwa na mazungumzo ya ufanisi na Putin na kushiriki katika mipango ya kimataifa, kama vile kupanua uhusiano na China na miradi kama vile upanuzi wa Haifa unaoongozwa na China. Hata hivyo, kwa sehemu kutokana na muundo wa kipekee wa mahusiano ya Marekani na Israeli, mbinu hii haiwezi kufua dafu. Tangu kutokea kwa tukio la Oktoba 7, sera ya mambo ya nje ya Israeli imekuwa ikiitegemea zaidi Washington, hasa kwa kuzingatia masuala ya usalama wa taifa.
Kwa upande mwingine, Trump anaingia kwenye muhula wake wa pili chini ya upinzani mkubwa kuliko ilivyokuwa mwaka 2017.
Kuna shauku kubwa kufahamu iwapo sera za Marekani zitabadilika kimataifa na kikanda, hasa katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro. Trump anaonekana kuanza awamu hii kwa nafasi nzuri zaidi. Msimamo huu ulioimarishwa huenda ukaathiri mtazamo wake kwa sera za kikanda, kwa kulenga mijadala inayozunguka vita ambavyo ameahidi kukomesha.
Kama kiongozi ambaye hapo awali alishirikiana na Netanyahu, Trump alikuwa na nafasi muhimu katika kupunguza kutengwa kwa eneo la Israeli, kuhamishwa kwa Ubalozi wa Marekani, kutambuliwa kwa mamlaka ya Israeli juu ya Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu, na azimio la Abraham. Bila shaka, vitendo hivi viliimarisha msimamo wa Netanyahu, na kumwezesha kuunganisha mamlaka.
Uhusiano mgumu na Netanyahu
Kutotabirika kwa Netanyahu kumemfanya kuwa mshirika asiyetegemewa wa marais wa Marekani, hasa pindi matarajio ya Israeli yanapotofautiana na maslahi ya Upinzani wa Marekani unapoinuka, anajiweka kama mtetezi wa maslahi ya Israeli, akishirikiana na umma wa Israeli. Wakati mahusiano yanapolingana, anaangazia jukumu lake la kimkakati katika kufikia matokeo mazuri.
Mbinu hizi mbili zimemsaidia Netanyahu kudumisha umaarufu bila kujali kama anatia dosari mahusiano. Kwa mfano, wakati wa kampeni yake ya uchaguzi wa 2019, alionesha ushirikiano wake na Biden na Putin, na baada ya Oktoba 7, alijionyesha kama mtu thabiti, licha ya kugombana na Biden kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza.
Netanyahu alitoa ahadi kadhaa kwa utawala wa Marekani, na kumfanya Biden kutangaza mpango wa kusitisha mapigano. Walakini, taarifa za Netanyahu kupinga masharti fulani ya mpango huu hivi karibuni zilimweka Biden katika hali ngumu. Zaidi ya hayo, Netanyahu alitoa matamshi mabaya katika kila mkutano. Kwa kuzingatia mtindo wa uongozi wa Trump, kuna uwezekano kwamba anaweza kuhimili mbinu za Netanyahu, zenye kulenga kuwaridhisha watazamaji wake wa ndani.
Ahadi ya kumaliza vita?
Bila kujali utawala au rais, kudorora kwa mahusiano ya Marekani na Israeli au kupunguzwa kwa usaidizi wa Marekani kwa Israel hakutarajiwi. Walakini, Trump sio kiongozi ambaye angevumilia kutendewa sawa na Netanyahu ambayo Biden alipata. Kwa maneno mengine, wakati muhula wa pili wa Trump huenda usiwe mzuri zaidi kwa Wapalestina, Netanyahu anaweza kukabiliwa na kipindi kigumu zaidi.
Dhima kuu ya Trump wakati wa kampeni yake ilikuwa ni kumaliza vita na hii inaweza kuwa ajenda yake kimataifa.
Kwa kuzingatia umaarufu wake katika mazungumzo ya kimataifa na kuongezeka kwa matarajio, utawala wa Trump unaweza kufuata hatua katika mwelekeo huu. Suala la kweli, hata hivyo, liko katika masharti ambayo mzozo wowote ungeisha-labda ni jambo gumu kwa Netanyahu.
Kupunguza misaada kwa Israeli
Kwa vyovyote vile, Trump anaweza kutumia msimamo wenye changamoto zaidi dhidi ya Trump wakati wa muhula wake wa pili. Ingawa Israeli haitarajiwi kufanya kazi kikamilifu chini ya mwelekeo wa Marekani, inaweza kutarajiwa kwamba itahisi shinikizo lililoongezeka.
Kwa upande wa Trump, kusitisha uungaji mkono wa Israeli, pia unaweza mbinu nyingine itakayofanya kazi.
Mwandishi wa maoni haya ni mchambuzi wa masuala ya Israeli katika Taasisi ya ORSAM.