Mamlaka ya Israeli imeizuia Umoja wa Mataifa kuingia kivuko kilichofungwa cha Rafah, kituo kikuu cha kuingiza misaada ya kibinadamu Gaza, Umoja wa Mataifa ulisema.
Jens Laerke, msemaji wa shirika la OCHA, alisema siku ya Jumanne, kuwa kulikuwa na akiba ya siku moja tu ya mafuta ya kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya Gaza iliyozingirwa.
"Kwa sasa hatuna uwepo wowote kwenye kivuko cha Rafah kwani ufikiaji wetu umekataliwa na COGAT," alisema, akimaanisha wakala wa Israeli ambao husimamia usambazaji wa vitu vinavyoingia Palestina.
"Tumeambiwa hakutakuwa na kuvuka kwa wafanyakazi au bidhaa ndani au nje kwa wakati huu. Hiyo itaathiri pakubwa kwa misaada mingi tuliyonayo.
Uhaba wa mafuta
"Kuna akiba ndogo ya kutosha siku moja pekee inayopatikana.
"Kama mafuta yanaingia tu kupitia Rafah, hio ni akiba ya siku moja ya operesheni Gaza nzima."
Kama hakuna mafuta yanayoingia, "itakuwa njia ya kugandamiza operesheni ya kibinadamu Gaza," alisema Laerke.
Sasa hivi njia mbili kuu za kupitisha misaada Gaza zimefungwa, akimaanisha kivuko cha Rafah kutoka Misri na kivuko cha Kerem Shalom kutoka Israel.