Almasi nyingi kutoka Namibia husafirishwa nchini Israel./Picha: AP

Nchi ya Namibia imejiunga na nchi nyingine duniani kuitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutambua vita vya Israeli huko Gaza kama mauaji ya halaiki.

Nchi hiyo ilienda mbali zaidi na kushinikiza kuwekwa kwa vizuizi dhidi ya Israel na makampuni yake. Hata hivyo, hili limeweka dosari katika biashara ya almasi kati ya Israel na Namibia, ambayo huwa na udhibiti mkubwa sana, na kuibua maswali kuhusu uwezo wa nchi hiyo inayopatikana kusini mwa Afrika katika kupunguza mateso ya wapalestina mjini Gaza.

“Rafiki wa wote asiye na adui,” ndivyo Namibia inavyojitanabaisha katika sera zake za nje, zilizopatikana baada ya uhuru wa nchi hiyo kutoka Afrika Kusini mwaka1990.

Kwa kiasi fulani, uhusiano kati ya Namibia na Israel umejaa kutokuaminiana kwani Israel ilikuwa miongoni mwa nchi chache zilizodumisha uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Licha ya hili, nchi hizo zimekuza uhusiano wa kibiashara kwa miaka mingi, huku almasi ikiwa ndio kiini.

Wito wa Amani

Katika taarifa yake ya Februari 24 katika mahakama ya ICJ, Waziri wa Sheria wa Namibia Yvonne Dausab alihusisha uwepo wa Israel kwenye ardhi ya Palestina na mapambano ya nchi yake dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini na mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na Ujerumani dhidi ya jamii za Nama na Ovaherero, katika karne ya 20.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, mwanasheria wa Namibia katika Mahakama hiyo , Phoebe Okowa, alipendekeza hatua kali zichukuliwe dhidi ya Israel.

Okowa alizitaka nchi nyingine kusitisha uhusiano wa kibiashara na Israel kuongeza shinikizo kwa Tel Aviv.

"Nchi zote zina wajibu wa kutotambua, kusaidia, au kuchangia katika kuendeleza kazi hiyo haramu ambayo inajumuisha wajibu wa mataifa ya tatu kutotoa msaada au usaidizi katika kudumisha hali hiyo haramu."

Wakati Namibia inatoa ambao si wa moja kwa moja wa kususia bidhaa za Israeli, inatilia shaka uhusiano wake wa kibiashara na Israel hasa katika almasi.

Ni dhahiri kwamba Namibia itashindwa kuongoza mfano katika kuweka zuio kwenye hizi biashara.

Vipi kuhusu almasi?

Mkurugenzi Mtendaji katika Wizara ya Madini na Nishati ya Namibia, Penda Ihindi, anasema asili ya uwekezaji wa Israel nchini Namibia haiwezi kutengwa na utaifa, akipendekeza kuwa kususia vilivyoidhinishwa na serikali au vikwazo vya biashara za Israel havitawezekana chini ya sheria za Namibia.

"Namibia inajiunga na biashara ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa," Ihindi anaiambia TRT World.

"Matokeo yake, Namibia haijifungi na hatua za upande mmoja kutatua maendeleo ya kijiografia na kisiasa duniani. Uwekezaji wote nchini unazingatiwa ndani ya masharti ya sheria ya uwekezaji na sera zinazohusiana.

Mwaka 2022, Namibia ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya dola milioni 59.82 kwenda Israel, nyingi zikiwa ni almasi. Kwa upande mwingine, bidhaa za kutoka Israel nchini Namibia zilifikia thamani ya dola milioni 3.8, hususani mashine za kung'arishia madini haya.

Israel imepata shinikizo kubwa ulimwenguni kutokana na kitendo chake cha kuishambulia Gaza./Picha: AP

Usawa chanya wa biashara ni jambo ambalo maofisa wa Namibia watakuwa na shida kujitolea hata kama wanachukua msimamo wa umma wa kuunga mkono Palestina, maafisa wanasema.

Almasi ndio bidhaa yenye kusafirishwa kwa wingi kutoka Namibia.

Ukaguzi wa hati za umiliki wa kampuni katika Mamlaka ya Biashara na Haki Miliki ya Namibia (BIPA) unaonesha anwani za biashara za kampuni nyingi zinazohusika na biashara ya almasi ya Namibia zimesajiliwa nchini Israeli.

Tuliameni Kalomoh, Naibu Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje (sasa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano), anaonya kuwa kauli ya Namibia katika ICJ inaweza kutilia shaka uaminifu wake kwa kuzingatia uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

"Kauli mbili zinaweza kuweka uaminifu wako mashakani. Mtu anaweza kufikiri kwamba kauli kama hiyo kama ile iliyotolewa na Waziri wa Sheria katika ICJ ingekuwa imetungwa au angalau kuhaririwa na Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ambayo ndiyo msimamizi wa sera ya mahusiano ya nje ya Namibia.

"Wakati wowote nchi inapotaka au kupendekeza vikwazo kama Namibia inavyofanya, inapaswa kuzingatia athari kubwa zaidi ambazo vikwazo vinaweza kuwa nazo, na katika kesi hii, vinaweza kuwa na madhara zaidi kwa Namibia kuliko ilivyo kwa Israeli," Kalomoh anaiambia TRT World, katika mahojiano.

Sio sawa kwa Waziri wa Sheria kutoa kauli kuhusu diplomasia ya kimataifa wakati kuna mamlaka inayotambulika kikatiba, anasema Kalomoh.

Kwa Namibia, kuitisha vikwazo vya kimataifa kwa Israel lakini kutokuwa na nia ya kusitisha uhusiano wake wa kibiashara kunatia shaka ukweli na uaminifu wake na kama inaweza kuchukuliwa kwa uzito na nchi nyingine, anasema Kalomoh.

Mahusiano ya ndani

Lev Leviev, Julius Klein, na Maurice Tempelsmann ni watu maarufu katika biashara ya almasi wenye maslahi ya kibiashara katika sekta ya almasi ya Namibia.

Kampuni za, Lev Leviev Diamonds, Julius Klein Diamonds, na Kaplan Lazar zinafanya kazi kwa ukaribu na kampuni ya Namibia Diamond, ikiwa imeajiri maeflu ya wanamibia katika viwanda vya kukata na kusafishia madini hayo.

Pia kuna kile kinachojulikana kama mtazamaji wa NDTC, ambayo ni kampuni iliyosajiliwa ya Namibia ambayo imepewa kandarasi ya kununua almasi ghafi kutoka NDTC kwa ajili ya kukata, kung'arisha, na kuongeza thamani nchini Namibia.

Lev Leviev na makampuni yake waliangaziwa kimataifa wakati kundi la Wapalestina lilipofungua kesi ya dola bilioni 34, wakidai anafaidika na makazi haramu ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Ripoti ya Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari za Uchunguzi (ICIJ) inaangazia ushiriki wa tasnia ya almasi katika kukalia kwa mabavu maeneo ya Wapalestina.

"Kesi iliyowasilishwa Washington DC inadai uhalifu mbalimbali chini ya sheria za Marekani na kimataifa, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, njama, utakatishaji fedha, ulaghai, uwongo na wizi," Ntibinyane Ntibinyane aliandika katika makala yake.

Kando na biashara ya almasi, kampuni ya kijeshi ya Namibia na kampuni ya Israel ya FK Generators and Equipment wanafanya kazi pamoja kujenga kituo cha umeme kinachoendeshwa na dizeli kiitwacho ‘Anixes II’ katika mji wa bandari wa Walvis Bay.

FK Generators ilipewa mkataba na kampuni ya umeme inayomilikiwa na serikali ya Namibia ya NAMPOWER kuendeleza kituo cha kitaifa cha kuhifadhi mafuta kwa ubia na kampuni ya kijeshi ya Namibia.

Kutoa wito wa vikwazo kwa makampuni ya kibinafsi ya Israeli nchini Namibia kunaweza kuonekana kama unyanyasaji.

Lakini ushirikiano wa kijeshi kati ya Israel na serikali ya Namibia uko kwenye taarifa ya Namibia yenyewe huko The Hague inayosema, "nchi zote zina wajibu wa kuhakikisha kwamba makampuni yaliyo chini ya mamlaka au udhibiti wao hayafanyi biashara ya bidhaa za Israeli au makampuni kutoka Israel”.

Hili linazua swali wakati Namibia inapotaka kugomewa na kuwekewa vikwazo kwa makampuni ya Israel kimataifa bila kudai hivyo ndani ya nchi, je, inapaswa kuchukuliwa kwa uzito na wengine?

Vitalio Angula ni mwandishi anayepatikana mjini Windhoek, Namibia @vita_angula

TRT Afrika