Maadhimisho ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda / Photo: AP

Mmoja wa watu wanaosakwa zaidi duniani kwa kutoroka baada ya kuhusika na mauaji ya halaiki nchini Rwanda, Fulgence Kayishema amekamatwa nchini Afrika Kusini baada ya kutoroka kwa miongo kadhaa, mamlaka nchini Afrika Kusini ilisema Alhamisi.

Kayishema, ambaye anatuhumiwa kupanga mauaji ya takriban wakimbizi 2,000 wa kabila la Kitutsi katika Kanisa Katoliki la Nyange wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya kabila la Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994.

Kayishema alikamatwa huko Paarl, eneo la magharibi la Cape nchini Afrika Kusini, siku ya Jumatano, kulingana na taarifa ya mahakama ya kimataifa.

Shirika la Kimataifa la Mabaki ya Mahakama za Jinai, IRMC, lilisema katika taarifa yake kuwa Kayishema alikamatwa katika operesheni ya pamoja ya mamlaka ya Afrika Kusini na timu ya mahakama hiyo ambayo inafuatilia waliotoroka.

Kayishema anashutumiwa kwa kupanga mauaji ya takriban wakimbizi 2,000 wa kabila ya Kitutsi wakati wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda mwaka 1994

Mahakama hiyo imesema Kayishema alikuwa mtoro kwa zaidi ya miaka 20 na "kukamatwa kwake kunahakikisha kwamba hatimaye atakabiliwa na haki kwa makosa yake ya uhalifu.

Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa nchini Rwanda mwaka 1994 katika siku 100.