Idadi ya watu wanaovuka mpaka wa kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa siku imeongezeka maradufu.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na wilaya ya Rubavu, uvukaji wa wati katika mpaka huo umeongezeka kutoka watu 4,000 hadi 20,000.
Kabla ya mlipuko wa ugonjwa Uviko-19, kati ya watu 40,000 hadi 50,000 walikuwa wakivuka mpaka huo wenye shughuli nyingi zaidi barani Afrika.
Kulingana na Meya wa wilaya ya Rubavu Prosper Mulindwa, hali ilibadilika baada ya kudhibitiwa kwa ugonjwa huo, na kufunguliwa kwa mpaka huo kwa upande wa Rwanda.
“Hali imerejea kuwa ya kawaida toka tulipoimarisha udhibiti dhidi ya magonjwa ya milipuko,” amesema.
DRC bado ni soko kubwa
Kulingana na Mulindwa, raia wengi kutoka DRC huingia nchini Rwanda kwa ajili ya kujipatia elimu, hasa kutoka vyuo vikuu vya nchi hiyo, hali inayodhihirisha ongezeko la shughuli za mpakani.
Vikwazo vya kibiashara mpakani
Licha ya DRC kuwa soko kubwa kwa bidhaa za Rwanda, bado kuna vikwazo vinavyosababishwa na mamlaka za DRC.