Mohamed Salah atakosa michezo miwili ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Misri baada ya kujeruhiwa Alhamisi katika mechi ya timu yake dhidi ya Ghana, ambayo ilitoka sare ya 2-2, hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira Misra EFA.
"Vipimo vya X-ray alivyofanya Salah vimethibitisha kwamba ana jeraha la mkononi na kwamba atakosa kuchezea timu yake katika mechi mbili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde na raundi ya 16 iwapo (Misri) itafuzu," imesema taarifa fupi ya EFA.
Mapema Ijumaa, daktari Mohamed Abu El-Ela wa Misri alisema, Salah awali alitaka kuendelea kucheza katika michuano muhimu lakini maumivu yalipozidi aliomba kuondolewa.
Ukubwa wa jeraha
Kwa upande wake, Meneja wa Salah wa Liverpool, Juergen Klopp, alisema mapema kwamba jeraha hilo linaweza kuwa kubwa, akisema mchezaji huyo ni nadra kuumizwa au kutoka mchezoni anapokuwa uwanjani.
"Nimezungumza nae jana usiku. Wanafanya vipimo zaidi na baadae tutajua zaidi," Klopp aliwaambia waandishi.