Ikiwa kwenye kipindi chake cha saba, Miezi saba, Podikasti mpya ya nyota huyo za zamani kutoka Nigeria, ikimshirikisha Chris Mchardy, gwiji wa michezo kutoka Uingereza, kama mwandalizi mwenza, imeacha simulizi na mishangao ya kutosha.
Katika kumuenzi mmoja wa wachezaji wake bora wa zamani, timu ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), tovuti ya Chelsea inamtaja Mnigeria huyo kama gwiji maaurufu anayejitoa kwa timu, kwenye nyakati ngumu na pekee.
Kama anavyoenziwa na klabu yake ya zamani, kwa sasa, Obi anakwenda hatua zaidi kwa kuanzisha Posikasti yake mpya ambayo inabua hisia na mishangao mingi, siku hadi siku.
Kwa mfano, jioni ya Disemba 18 mwaka jana, mwanasoka huyo wa zamani alimualika aliyekuwa Kocha wake wakati anahudumu na Chelsea, Jose Mourinho,
Maarufu kama ‘Binadamu wa Pekee', mkufunzi huyo kutoka Ureno na kocha wa As Roma kwa sasa, alizikebehi baadhi ya timu zinazoshirikishi EPL, ikiwepo Tottenham Hotspur na Manchester United, alizofundisha kwa nyakati tofauti.
Akiwa ametundika daluga mwaka 2022, ilimlazimu Obi kuwa na akiba ya kutosha ya habari na matukio yahusuhuyo ligi hiyo maarufu duniani ili asiyembishwe wala kuachwa kwenye mataa na mkufunzi huyo machachari duniani.
Katika kipindi hicho, kilichodumu kwa saa moja, Obi alidhihirishia ulimwengu ukomavu wake katika kuandaa Podikasti toka tarehe 30, Oktoba.
Pengine, haikuwa kwa bahati kwamba jina la kipindi chake kilifanana na "Obi-Wan Kenobi", mhusika mkuu wa tamthiliya maarufu wa filamu ya Star Wars.
Kwa Obi na mwenzake Chris McHardy, malengo ya kipindi hicho ni kuwakaribisha na kuanzisha mazungumzo ya kuvutia na nyota wa soka, wasimamizi na wadau wengine wa kandanda duniani.
Mazungumzo ya kusisimua
Mbali na kabumbu lenyewe, kipindi hicho pia huangazia na kumulika tusiyoyejua ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo. Toka kianze Oktoba mwaka jana, Podikasti hiyo imekuwa na sehemu saba na mbili za nyongeza, ambazo zimejikusanyia mamilioni ya wasikilizaji.
Baadhi ya sehemu za Podikasti zinazoandaliwa na Obi zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii kama vile Spotify, Apple Podcasts, Google Podcasts, YouTube na nyinginezo.
Kila sehemu za Podikasti hizo hudumu kwa saa moja mpaka mawili.
Kwa namna ya pekee, Obi alimkaribisha nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Unigereza, aliyepata kuhudumu naye pale Chelsea.
Kama bahati, mgeni wake wa pili alikuwa Frank Lampard, ambaye pia alikuwa nahodha wa mabingwa hao wa Kombe la Dunia kwa Mwaka 1966, na pia mchezaji mwenza pale Chelsea.
Katika sehemu za vipindi vilivyofuata, Obi alikuwa mwenyeji kwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika Victor Osimhen, winga wa zamani wa Ufaransa Florent Malouda na mshambuliaji wa zamani kutoka Italia, Gianfranco Zola.
Mbali na Mourinho, Obi amewahi pia kumuhoji Kocha wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Matteo.
Maoni ya kutia moyo
Tayari Podikasti ya Obi imeanzakukubali kwa wasikilizaji na watazamaji.
Baadhi, wamediriki hata kuilinganisha na majukwaa makubwa ya kimichezo kama vile ESPN FC, Football Ramble na Podikasti inayoandaliwa na mchezaji Peter Crouch.
Hata vyombo vya habari vikubwa Uingereza vimekuwa vikinukuu baadhi ya sehemu za Podikasti ya Obi Major na baadhi ya dondoo zake zimevutia mamilioni ya watumiaji wa mitandao ya jamii duniani.
Japo matarijio kwa Obi, ambaye amepata kuichezea Stoke FC na Middleborough za Uingereza, Trabzonspor ya Uturuki, na vilabu vya Norway na Uchina ni makubwa, ni suala la muda tu, kwa gwiji huyo kutoka Nigeria kucheka na nyavu.