Kocha wa Nigeria Jose Peseiro alimsifu Victor Osimhen "mshupavu sana" kwa mwanasoka bora wa Afrika mwaka huo aliyecheza bila kuchoka wakati Super Eagles ilipoilaza Cameroon 2-0 kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi.
"Hakufunga lakini alikuwa na mchezo mzuri sana. Si rahisi kumzuia mtu huyo," kocha wa Ureno Peseiro alisema kufuatia mechi ya hatua ya 16 bora mjini Abidjan.
Ademola Lookman alifunga mabao yote mawili, lakini Osimhen alimuandalia la kwanza na mbio zake za ajabu na ukandamizaji zilizua matatizo ya mara kwa mara kwa safu ya ulinzi ya Cameroon.
Tahthmini ngumu sana
"Waulize mabeki wa timu pinzani waliteseka kiasi gani. Bao la kwanza, alitengeneza yeye. Ni mzuri kwa timu yetu," Peseiro aliongeza.
"Hakuna mtu anayeweza kushinda mechi peke yake, kila mtu anapaswa kucheza, lakini yeye ni mfano mzuri."
Mabingwa mara tatu Nigeria sasa wanafuzu kwa robo fainali siku ya Ijumaa dhidi ya Angola, na bado haijafahamika iwapo kipa Stanley Nwabili ataweza kucheza mchezo huo baada ya kutolewa kwa machela kwenye mechi dhidi ya Cameroon.
"Haiwezekani kutathmini hali mara moja. Tunahitaji saa 24-48 kabla ya kujua, lakini ikiwa hawezi kupona tutacheza na kipa mwingine," Peseiro alisema.
Kuhusu Angola, walioongoza kundi lao na kisha kuishinda Namibia 3-0 katika hatua ya 16 bora siku ya Jumamosi, Peseiro aliongeza: "Ni timu nzuri sana. Nadhani katika wakati huu, timu zote zinaweza kushinda mashindano haya.
"Angola wamefanya vizuri sana, na kama tunataka kuwashinda ni lazima tufanye kila tuwezalo, kama leo."