Yevgeny Prigozhin anasema kwenye video kwamba wanaume wake wanapaswa kuwa na tabia nzuri kwa wenyeji wa Belarusi / picha: Reuters

Mkuu wa kikundi cha mamluki cha Wagner Yevgeny Prigozhin, ameonyeshwa kwenye video akiwaambia wapiganaji wake kwamba hawatashiriki zaidi katika vita vya Ukraine kwa sasa, lakini akiwaamuru kujimudu na kujitayarisha kwa ajili ya Afrika.

Mataifa ya Magharibi wametafsiri uasi wa kiongozi wa Wagner dhidi ya rais Putin, Juni 23-24 kama changamoto kwa utawala wa Rais Vladimir Putin.

Wamedai uasi huo unaonyesha udhaifu wa rais Putin na changamoto ya vita yake dhidi ya Ukraine.

Kanda hiyo, iliyochapishwa tena na huduma yake ya vyombo vya habari kwenye Telegram siku ya Jumatano, ni ushahidi wa kwanza wa video wa mahali alipo Prigozhin tangu usiku wa uasi.

Katika video hiyo, (uhalisi wake haujathibitishwa), mtu ambaye sauti yake na Kirusi unasikika na kufanana na ya Prigozhin.

Ilirekodiwa baada ya giza kuingia, ingawa inawezekana kutambua umbo la Prigozhin akiwa na kikundi cha wanaume.

Safari ya Afrika

Video hiyo iliyotumwa Jumatano ikionyesha Prigozhin akipokea bendera nyeusi ya Wagner, iliyopambwa kwa kauli mbiu "Damu, heshima, Nchi ya Mama, Ujasiri", kutoka kambi yao kusini mwa Urusi.

Prigozhin anasema kwenye video kwamba wanaume wake wanapaswa kuwa na tabia nzuri kwa wenyeji na kuwaamuru kukusanya nguvu zao kwa "safari mpya ya Afrika."

"Na labda tutarejea kwa operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine wakati fulani, wakati tuna uhakika kwamba hatutalazimika kujiaibisha," Prigozhin alisema.

Wagner ilianzishwa na Prigozhin na Dmitry Utkin, afisa wa zamani wa kikosi maalum katika ujasusi wa kijeshi wa GRU wa Urusi, kama njia ya Urusi kujihusisha na vita katika nchi zikiwemo Syria, Libya na Mali ambazo haziwezi kukanushwa kabisa.

Wagner iliisaidia Urusi kutwaa eneo la Crimea mwaka 2014, ikapambana na wanamgambo wa Daesh nchini Syria, waliokuwa wakiendesha harakati zao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mali na kuuchukua mji wa Bakhmut wa Ukraine kwa niaba ya Urusi mapema mwaka huu.

TRT Afrika