Mashambulizi katika hospitali ya Al Ahli huko Gaza yamelaaniwa na viongozi tofauti duniani / Picha: Reuters

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa , Antonio Gutteres amelaani mashambulizi siku ya Jumanne katika hospitali ya Kianglikana ya Al Ahli huko Gaza, huku kukiwa na ripoti za zaidi ya watu 500 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakiwemo wanawake na watoto.

"Nimeshtushwa na mamia ya watu waliouawa katika hospitali ya Al Ahli huko Gaza," Gutteres amesema katika hotuba ambayo alitoa akiwa Uchina.

"Ninatoa wito wa usitishaji mapigano wa haraka wa kibinadamu ili kutoa wakati na nafasi ya kutosha kusaidia kutimiza maombi yangu mawili na kupunguza mateso makubwa ya wanadamu tunayoshuhudia," Gutteres ameongezea.

Gutteres pia analaani shambulizi dhidi ya shule ya UNRWA mapema leo katika kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi huko Gaza na kusababisha vifo vya takriban watu sita.

"Hospitali, zahanati, wafanyakazi wa matibabu, na majengo ya UN yanafaa kulindwa chini ya sheria za kimataifa,''Gutteres amesema katika taarifa.

TRT Afrika