Katibu Mkuu, Jumuiya ya Afrika Mashariki Peter Mathuki | Picha: EAC

Alikanusha kwamba Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF), ambalo lilipelekwa katika eneo lenye matatizo mwishoni mwa mwaka uliopita, lilishindwa katika majukumu yake.

"Hali sio kama ilivyokuwa kabla ya wanajeshi kutumwa huko," alisema, akisisitiza kuwa alikuwa anatafuta kukomesha uhasama katika kipindi cha miezi michache.

Aliongeza kuwa EACRF inaunga mkono na baraka za nchi washirika katika jumuiya hiyo na haipaswi kuonekana kama jeshi lisilo halali.

"Jukumu lake ni kuhakikisha amani inarejeshwa DRC," alisema, akielezea kuwa EAC imeanzisha mikakati miwili - ya kisiasa na kijeshi - kuhakikisha hali inarudi kawaida katika taifa kubwa zaidi la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwenye upande wa kisiasa, EAC ilimteua Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kama msuluhishi. Amejukumiwa kushirikisha wadau wote katika kutafuta amani.

Njia ya kijeshi imeona wanajeshi kutoka nchi nne kati ya nchi saba washirika wakipelekwa chini ya EACRF: Kenya, Uganda, Sudan Kusini, na Burundi.

Tanzania, Uganda na Kenya wamefanya zaidi ya hayo; wametoa michango kwa ajili ya mchakato wa amani, pamoja na nchi za Angola, Senegal, na Gabon.

Tume ya Umoja wa Afrika (AU) hivi karibuni ilitoa dola milioni 2 kwa Mfuko wa Amani wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, na Sweden pia wamefuata mfano huo.

Wakati SG akiwaelezea waandishi wa habari juu ya juhudi zilizoendelea za kurejesha amani Mashariki mwa Kongo, habari zilisambaa kuhusu mvutano mpya kati ya Rwanda na DRC na kuingilia kati kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Mathuki alisisitiza kuwa EAC itaendelea na diplomasia katika kushughulikia mgogoro huo kwa kushirikisha viongozi wa nchi ili kurejesha amani.

TRT Afrika