Mji wa San Francisco una wakazi 46,000 wenye asili ya weusi. / Picha: AA  

Wasimamizi wa mji wa San Francisco wanalenga kuiomba msamaha jamii wa watu weusi baada ya miongo ya sheria na sera zilizokuwa zinawabagua.

Maofisa hao wamepanga kupitisha azimio la kuiomba radhi jamii hiyo pamoja na wajukuu zao. Wanachama wote 11 wamejiandikisha kama wafadhili, na kuhakikisha kupitishwa kwake, na hivyo kuifanya San Francisco kuwa kati ya miji ya kwanza nchini Marekani kufanya hivyo.

Azimio hilo linautaka mji wa San Francisco kutorudia utekelezaji wa sera na vitendo vinavyomkandamiza mtu mweusi ndani ya jamii zao. Mji wa San Francisco una wakazi 46,000 wenye asili ya weusi.

“Msamaha huu ni wa muhimu sana na sio tu ishara ya kukubali kosa na kufanya mabadiliko,” alisema mmoja wa wasimamizi aitwaye Shamann Walton, ambaye ni mjumbe pekee mwenye asili ya kiafrika, katika kamati inayosikiliza azimio hilo, mwanzoni mwa mwezi huu.

Malipo taslim

Wengine wanasema kuwa msamaha huo pekee yake hautoshi kama fidia.

“Msamaha ni sawa sawa na kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa,” anasema Mchungaji Amos C. Brown, mjumbe wa kamati ya fidia iliyopendekeza kuwepo na mpango wa kuiomba msamaha jamii hiyo. “ Tunachohitaji ni hatua madhubuti.”

Msahama huo utakuwa ni moja ya fidia zilizopendekezwa kati ya mapendekezo 100 yalioandaliwa na kamati ya mji huo.

Kamati hiyo, pia ilipendekeza kuwa ila mtu mzima mweusi aliyekidhi vigezo kupatiwa dola milioni 5 na kuhakikishiwa malipo ya kila mwaka ya takriban dola 100,000 kuziba pengo kubwa la umiliki mali kati ya watu weusi na weupe.

Hata hivyo, hatua za juu kuhusu mapendekezo hayo zimekosekana. Meya wa London Breed, ambaye ni Mweusi, amesema anaamini fidia zinapaswa kushughulikiwa katika ngazi ya kitaifa.

Watu weusi kuwa nyuma

Meya huyo aliamua kuondoa dola milioni 4 katika mpango huo, kufuatia ufinyu wa bajeti.

Wanaharakati wa ulipaji fidia katika kesi iliyotangulia walionyesha kuchoshwa na kasi ndogo iliyooneshwa na serikali, wakisema kuwa wakazi weusi wanaendelea kulegalega katika vipimo vinavyohusiana na afya, elimu na mapato.

Asilimia 38 ya watu weusi ,mjini San Francisco hawana makazi, pamoja na kuwa ni sehemu ya asilimia 6 ya idadi ya watu, kulingana na sensa ya mwaka 2022.

California ilikuwa jimbo la kwanza kuandaa kikosi kazi cha kulipa fidia mwaka 2020. Kamati hiyo ilivunjwa mwaka 2023, na ikaja na mapendekezo kadhaa ya kisera ikiwemo kuwepo na njia za kukokotoa malipo ya pesa taslimu kwa wazao wa watumwa.

Historia ya ubaguzi

Lakini miswada ya fidia iliyoletwa na Baraza la Wabunge Weusi la California mwaka huu pia huacha usuluhishi wa kifedha, ingawa kifurushi hicho kinajumuisha mapendekezo ya kuwalipa fidia watu ambao serikali ilinyakua ardhi yao kupitia eneo maarufu, kuunda wakala wa malipo ya serikali, kusitisha kwa kazi za kushurutisha na uombaji msamaha.

Majimbo mengine pia yameomba radhi kutokana na historia yake ya ubaguzi na vurugu zilizopelekea watu weusi kuingia utumwani, kulingana na azimio hilo.

Mwaka 2022, Boston ilkuwa jiji la kwanza nchini Marekani kuomba msamaha. Mwaka huo huo, halmashauri ya Jiji la Boston ilipiga kura kuunda kikosi kazi cha ulipaji fidia.

TRT Afrika