Wakimbizi wa Sudan wakikimbilia kusaka hifadhi nchini Chad/ Picha: Reuters

Na Yassmin Abdel- Magied

Kengele za hatari kuhusu el-Fasher, Darfur zimeanza kulia siku chache tu, kabla ya kuingia mwaka wa pili wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Sudan.

Kukiwa na hofu kuwa mji huo utatumbukia katika machafuko makubwa, Umoja wa Mataifa unaonya kuwa zaidi ya raia 800,000 wako katika hatari kubwa ya mashambulizi ya ghafla, ikiwemo uchomwaji moto wa vijiji.

Takribani nusu milioni ya wakimbizi na watu wasio na makazi wanatafuta hifadhi kaskazini mwa Darfur, wakiwa na wasiwasi juu ya maisha yao.

Wataalamu wanasema kuwa matumaini ya kumaliza mauaji ya watu yanazidi kufifia. Kulingana na Nathaniel Raymond, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kibinadamu ya Yale, hatari ya machafuko hayo ni ya kiwango cha "Hiroshima na Nagasaki."

Akizungumza na waandishi wa habari, aliongeza, "Hii si hali nzuri kabisa." Ni mapambano ya mwisho kwa Darfur, wakati ambapo RSF inalenga kumaliza mauaji ya 2004/2005," anasema Raymond.

Macho yaliyofumbwa

Sanduku la mauaji. Mauaji ya viwango vya Hiroshima na Nagasaki. Takribani watu milioni moja wapo katika hatari ya kuuwawa. Maneno haya yanaonekana magumu kueleweka, ya kushangaza na kutisha. Hata hivyo, mauaji yanainyemelea Darfur, na dunia inafumbia macho.

RSF inaelekea kuibua janga lingine la ghasia, kwani kundi hilo limefanya mara kwa mara, lakini wasiwasi wa ukatili huo usioelezeka unaleta zaidi ya taarifa za vyombo vya habari na "kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano." Huku si kuleta kisu kwenye mapigano ya bunduki, hii ni kutuma faksi ili kujilinda dhidi ya ndege isiyo na rubani.

"Inaumiza sana kuona kiwango kikubwa cha upuuzaji kutoka jumuiya ya kimataifa kuhusu Sudan," anasema Hala al-Karib, Mkurugenzi wa Kanda wa mtandao wa SIHA.

Maneno yake yanaakisi hisia za watu wa Sudan. Kuwa Msudan ni kuhisi kama mtu anaomba omba omba kila wakati. Mgogoro huo wa mwaka mzima tayari umepewa jina la "Vita Iliyosahaulika" na makampuni mengi ya vyombo vya habari na waangalizi.

Ni kwanini tumepuuzwa, tumekuwa kama wakati uliopita, wakati vita vinaendelea kurindima katika hali ya kutisha?

Kukwama kwa michango

Kwa sasa, Sudan ni chanzo cha mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani, lakini haina uwezo wa kukusanya fedha za kulisha mamilioni ya watu wanaokabiliana na makucha mabaya ya njaa.

Katika mkutano wa Ufaransa mwezi huu ulioangazia mwaka mmoja wa machafuko ya Sudan, wahisani waliahidi kuchangia zaidi ya dola bilioni 2 kama msaada.

Kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa Kholood Khair anavyoeleza, mengi ya haya yalitokana na ahadi za awali ambazo hazijatekelezwa. Hata hivyo, "isingekuwa kwa mkutano wa ahadi wa Paris, kungekuwa na pesa kidogo hakuna kitu kingefanyika kwa Sudan hata kidogo," anasema Khair.

Mkutano huo ulitawala kwenye vyombo vya habari, lakini kwa mara nyingine tena, masaibu ya Sudan yalizama kwenye giza.

Kuna sababu kadhaa kwanini machafuko hayo hayajapewa uzito kimataifa, ingawa sio lengo langu kwa sasa.

Wakati wa kuchambua—kuuliza kwa nini hili linafanyika—sio sasa. Mazungumzo hayo ni mbinu ya kuchelewesha, inayotumika tu kutatiza na kuvuruga kazi ya dharura iliyo mbele yetu.

Lazima hatua za haraka zichukuliwe.

Hatuwezi kusema hatukuonywa. Hata kama watu watatafuta njia za kusalia hai - na watafanya hivyo, kwa sababu Wasudan si kitu kama si watu wabunifu, wastahimilivu, jasiri - jumuiya ya kimataifa lazima ifanye sehemu yake.

Maombi yasiyo na meno hayana nguvu yoyote dhidi ya wanaume walio na mashine iliyoundwa kuua. Kujiinua, uwajibikaji na matokeo ndio njia pekee za kusonga mbele.

Mpango kazi

Je, nini kifanyike? Katika muda mfupi ujao, kuna wito kwa Marekani kuandaa kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kutafuta azimio la kutishia vikwazo dhidi ya wasambazaji wa silaha na wafadhili wa RSF.

Shinikizo lazima liwekwe kwa washirika wa RSF kuacha kuvipa silaha jeshi la wanamgambo kwa sababu haliwezi kuendelea na juhudi zake za vita bila msaada wa wahusika wa kimataifa.

Pili ni kushughulikia suala la njaa inayokuja sambamba na kuzidisha majanga ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kuzuka kwa kifua kikuu na magonjwa mengine ya kuambukiza katika kambi za watu waliokimbia makazi yao nchini kote.

Wanawake wa Sudan wakiandamana mitaani dhidi ya jeshi la nchi hiyo (AFP).

Ni vyema shinikizo liwekwe kwa pande zinazohasimiana kuruhusu misaada ya kibinadamu kwa maeneo yalioathirika zaidi.

Mbali na wajumbe wengi wa misaada ya kibinadamu, ufadhili lazima upatikane kwa Vyumba vya Kukabiliana na Dharura (ERRs) kote nchini, kutoa chakula kwa makumi ya maelfu ya raia wanaosubiri vita.

Usitishaji vita wa kudumu, ujenzi wa taifa, usalama wa watu. Kupata ahadi ya Mapinduzi Matukufu ya Disemba, pamoja na serikali ya kiraia, na kuwarudisha wanajeshi kwenye kambi. Haya ndio malengo ya mwisho.

Lakini kwa kuzingatia yote tunayojua, matamanio ya juu kama haya huhisi mbali sana, kama sayari kwa mbali.

Ndoto hiyo inaweza kutimia. Inabidi tufanye kila tuwezalo ili kutoruhusu watu wengine wa Sudan wafe.

TRT Afrika