Rohey Malick Lowe est maire de Banjul depuis mai 2018. Photo : Rohey Malick Lowe / Twitter

Meya pekee mwanamke wa Gambia, Rohey Malick Lowe amechaguliwa tena kushika wadhifa wake, katika uchaguzi wa umeya uliofanyika Mei 20 katika mji mkuu, Banjul.

Lowe, mwanachama wa upinzani, United Democratic Party (UDP) alimshinda mgombea mteule wa Rais Adama Barrow Eboy Faye.

Uchaguzi huo ulishuhudia chama tawala cha National People’s Party (NPP) kikifanya vibaya huku UDP pia ikishinda kinyang’anyiro cha umeya katika manispaa yenye watu wengi zaidi nchini.

Matokeo hayo yalikuwa pigo kwa Bw. Barrow, kwani miji mikubwa na mikoa sasa iko mikononi mwa upinzani. Eboy Faye ambaye alipoteza kwa Rohey Malick amempongeza.

Aliandika kwenye mtandao wa kijamii, ‘’Watu wa Banjul wamezungumza, wakiweka imani yao kwako kuliongoza jiji letu katika siku zijazo.’’ ‘’Nataka kueleza heshima yangu kubwa kwa uamuzi wa Wabanjulia,’’ anaongeza.

Rais pia amewapongeza washindi wote na kuahidi kuzingatia maendeleo na kuimarisha amani na utulivu nchini Gambia.

TRT Afrika