Boti ya doria ya nchini Hispania ikiwasili katika mji wa bandari wa Nouadhibou, Mei mwaka 2006./Picha: Reuters

Watu 15 na wengine zaidi ya 150 hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imebeba abiria 300 kuzama karibu na mji mkuu wa Mauritania wa Nouakchott siku ya Jumatatu, shirika la kimataifa la uhamiaji la IOM lilisema siku ya Jumatano.

Njia ya bahari ya Atlantiki kutoka pwani ya Afrika Magharibi kuelekea kisiwa cha Canary, hutumiwa zaidi na wahamiaji kutoka Afrika katika jitihada zao za kufika nchini Hispania, hutumika zaidi kipindi cha majira ya joto.

Shirika la IOM lilisema kuwa vikosi vya doria vya Mauritania viliokoa watu 120, kumi kati ya hao wakipelekwa hospitalini.

Kulingana na IOM, abiria hao walikuwa wanatokea Gambia na walikuwa wamekwisha tumia siku saba baharini kabla na kukumbwa na ajali hiyo.

Ibba Sarr, mchuuzi wa samaki mjini Nouakchott, alisema kuwa pepo kali zilizoshuhudiwa ndani ya siku mbili, zilisaidia kusogeza milli zaidi ya 30 karibu na fukwe.

"Kwa hali ilivyo, miili zaidi itapatikana ndani ya siku mbili," Sarr aliiambia Reuters kwa njia ya simu.

Chombo hicho kilipatikana mita zaidi ya 400, kaskazini mwa soko hilo, alisema.

Mamlaka za nchini Mauritania hazikuwa tayari kujibu maswali ya Reuters kufuatia ajali hiyo .

Zaidi ya wahamiaji 19,700 walifika katika pwani ya Canary kwa kutumia bahari ya Atlantiki kati ya Januari 1 na Julai 15, 2024, ikiwakilisha ongozeko la asilimia 160, ikilinganishwa na mwaka uliopita, shirika la IOM limesema.

Takribani wahamiaji 5,000 walipoteza maisha majini ndani ya miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2024 wakijaribu kufikia eneo la Hispania, mwezi Juni.

TRT Afrika
Reuters