Waasi wa M23 waliingia mjini Goma siku ya Jumatatu / Picha: AFP

Miili ya watu waliouawa ilitawanywa katika mitaa ya Goma na wagonjwa waliokuwa na majeraha ya risasi walijaa hospitali, siku moja baada ya waasi wanaoungwa mkono na Rwanda kuandamana katika mji mkubwa zaidi Mashariki mwa Congo, Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada yalisema Jumanne.

Waasi wa M23 waliingia mjini Goma siku ya Jumatatu huku wakiendelea kukabiliana na upinzani kutoka kwa jeshi la DRC.

Milio ya risasi iliendelea kusikika mitaani siku ya Jumanne ambapo maiti nyingi zilionekana, alisema Jens Laerke, Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na misaada (OCHA), akinukuu taarifa kutoka kwa wafanyakazi katika jiji hilo.

"Hali ya raia ndani na karibu na mji wa Goma bado inatia wasiwasi," Laerke aliuambia mkutano wa Geneva. "Hospitali za Goma zinashindwa kuwahudumia watu, zikijitahidi kudhibiti idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa," aliongeza.

Alisema pia kuna taarifa za ubakaji.

Mamia ya watu wamelazwa hospitalini wakiwa na risasi na majeraha mengine, alisema Adelheid Marschang, mratibu wa dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa DRC, siku ya Jumanne.

Shirika la Msalaba Mwekundu lilisema kuwa moja ya hospitali zake ilikuwa imepokea zaidi ya wagonjwa 100 ndani ya saa 24 wakiwa na majeraha ya kichwa na majeraha ya kifua kutokana na chokaa na vipande vya vigae.

"Na wakati hospitali imezidiwa, bado tunapokea simu kutoka kwa majeruhi waliokata tamaa ambao wanatatizika kupata huduma za afya," alielezea Patrick Youssef, Mkurugenzi wa kanda ya Afrika katika shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC).

"Cha kusikitisha sana, tumeona ongezeko kubwa la watoto waliojeruhiwa vibaya," alisema. Wagonjwa wanasubiri kwenye ushoroba kwa kukosa vitanda huku maegesho ya magari ya hospitali yakiwa yamegeuzwa kuwa kituo cha watu kupata matibabu, aliongeza.

Mapigano hayo yamesabisha kuongezeka kwa uporaji. ICRC na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wanasema kumekuwa na uporaji wa vifaa vya matibabu na chakula.

"Kipindi kunakuwa na vurugu, usambazaji wa chakula katika jiji unaweza kuathiriwa sana," Shelley Thakral, Msemaji wa WFP katika mji mkuu Kinshasa alisema.

TRT Afrika