Khartoum

Marekani imewahamisha wafanyakazi wa ubalozi huo na familia zao kutoka mji mkuu wa Sudan Khartoum, ambako mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces (RSF) ambayo yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Wito huo wa Marekani unakuja saa chache kabla nchi kama Qatar, Saudi Arabia na Ufaransa kuanza ondoa raia wao walio kubana na vita huko Sudan.

"Nimeamrisha, jeshi la Marekani lifanye operesheni ya kuwaondoa wafanyakazi wa serikali ya Marekani kutoka Khartoum," Rais Joe Biden alisema katika taarifa yake Jumapili.

RSF ilithibitisha katika ujumbe wa Twitter kwamba iliratibu na ujumbe wa kijeshi wa Marekani uliojumuisha ndege sita "kwa ajili ya kuwahamisha wanadiplomasia na familia zao Jumapili asubuhi."

Biden aliwashukuru wanadiplomasia na wanajeshi wa Marekani kwa juhudi zao nchini Sudan, na akasema "anapokea ripoti za mara kwa mara ... kuhusu kazi yao inayoendelea ya kuwasaidia Wamarekani nchini Sudan, kwa kadiri inavyowezekana."

"Vurugu hizi mbaya nchini Sudan tayari zimegharimu maisha ya mamia ya raia wasio na hatia. Izi vurugu lazima zikome, "alisema.

"Pande zinazopigana lazima zitekeleze usitishaji mapigano mara moja na bila masharti, kuruhusu ufikiaji usiozuiliwa wa kibinadamu, na kuheshimu matakwa ya watu wa Sudan."

Siku ya Jumamosi, mapatano ya saa 72 yaliyokubaliwa na jeshi la Sudan na RSF yalishindikana, huku mapigano yakizuka Khartoum na maeneo mengine kadhaa, ikiwa ni pamoja na miji ya karibu ya Bahri na Omdurman.

Sasa katika wiki ya pili, mzozo mbaya wa madaraka kati ya jeshi la Sudan na RSF umeua zaidi ya watu 400, huku wengine zaidi ya 3,500 wakijeruhiwa, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

AA