Hofu ya njaa imetatiza ugawaji wa chakula /Picha: AFP  

Mapigano yamezuka siku ya Jumapili kati ya Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF katika majimbo ya Khartoum, Al Jazirah na White Nile na katika mji wa El Fasher, mashuhuda wamesema.

Kulingana na mashuhuda hao, jeshi lilitekeleza mashambulizi ya angani katika eneo walipokuwa wamekusanyika wanamgambo wa RSF katika eneo lililo jirani na kiwanda cha kuchakata mafuta cha Jaili, kilicho kaskazini mwa Khartoum.

Wanamgambo wa RSF wanashikilia maeneo mengi ya mji wa Bahri, ikiwemo kiwanda cha Jaili wakati Jeshi la Sudan limekita kambi katika vitongoji vya kaskazini mwa Bahri na bohari za silaha za Hattab na Kadroo.

Ndege za kijeshi zilifanya mashumbulizi katika maeneo ya kusini mwa Sudan na katika wilaya ya Alkotainh ndani ya jimbo la White Nile, kulingana na mashuhuda.

Kamati za Upinzani za Wad Madani zilisema katika taarifa yake kwamba ndege za kijeshi zilifanya uvamizi dhidi ya mikusanyiko ya RSF katika kijiji cha Bika, magharibi mwa mji wa Wad Madani, mji mkuu wa jimbo la Jazirah.

Kilele: El Fasher

RSF imedhibiti miji kadhaa katika jimbo la Jazirah, tangu Disemba mwaka jana, ikiwa ni pamoja na Wad Madani. Mashuhuda wanasema kuwa mapigano pia yalianza tena kati ya jeshi na RSF kaskazini na mashariki mwa El Fasher yakihusisha silaha nzito.

Waliongeza kuwa jeshi lilianzisha mashambulizi ya anga kwenye mikusanyiko ya RSF mashariki mwa El Fasher.

Siku ya Jumapili, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) lilitangaza kuwa mapigano yalianza tena Jumamosi kati ya jeshi la Sudan na RSF katika vitongoji kadhaa vya magharibi na kusini mashariki mwa El Fasher, na kusababisha familia 250 kukimbia makazi yao na watu kudhaa kujeruhiwa .

Hakuna aliyetoa kauli yoyote hadi sasa, kati ya jeshi la Sudan na RSF.

Mapigano Sudan

Tangu Mei 10, El Fasher ameshuhudia mapigano kati ya jeshi, likiungwa mkono na vuguvugu lililotia saini makubaliano ya amani, na RSF, licha ya onyo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu mapigano katika mji huo, ambao unatumika kama kitovu cha operesheni za kibinadamu.

Kumekuwa na ongezeko la wito kutoka kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kuepusha maafa ya kibinadamu ambayo yanaweza kusababisha mamilioni ya watu kukumbwa na njaa na vifo kutokana na uhaba wa chakula unaosababishwa na mapigano hayo, ambayo yameenea hadi majimbo 12 kati ya 18 ya nchi hiyo.

Wito wa hivi karibuni kutoka UNICEF unataka kusitishwa mara moja mapigano nchini Sudan "ili kuepusha baa la njaa na uwezekano wa kupoteza maisha ya watoto."

Tangu katikati ya mwezi Aprili mwaka jana, Jeshi la Sudan na RSF zimefanya mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 15,000 na kugeuza zaidi ya watu milioni 8 wakimbizi, kulingana na Umoja wa Mataifa.

AA
TRT Afrika