Kongamano na maonyesha ya Uturuki na Afrika linafanyika Istanbul - Picha ya TRT Afrika

Na Ebubekir Yahya

Kongamano kubwa la kimataifa la biashara limefunguliwa katika mji wa Uturuki wa Istanbul linalolenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Uturuki na Afrika.

Kongamano la biashara barani Afrika na maonyesho yanaleta zaidi ya makampuni 40 ya Uturuki yanayoonyesha bidhaa na huduma zao katika sekta za nguo, vinywaji, teknolojia, nishati na elimu pamoja na huduma za ushauri wa kibiashara na kifedha.

Hafla hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki na Afrika (TABA) na kufadhiliwa na kampuni ya Uturuki ya Beam na Benki ya NCBA ya Kenya, ilianza Jumanne huku washiriki wakisisitiza umuhimu wa uhusiano unaokua kati ya Uturuki na nchi za Afrika.

Kiwango cha biashara kati ya Uturuki na Afrika kimeongezeka/ Picha : TRT Afrika

"Uturuki ni eneo la kimkakati. Ukiangalia Ulaya, Asia na Afrika, unaweza kupata maafikiano ya kimkakati kati ya pande zote tatu, ambayo ni Istanbul,” rais wa TABA Fatih Akbulut aliambia mkutano.

Kiwango cha biashara kati ya Uturuki na Afrika kimeongezeka hadi takriban dola bilioni 30 kwa sasa kutoka dola bilioni 4.5 mwaka 2005 huku uwekezaji ukistawi kutoka pande zote mbili, Akbulut alisema.

Uturuki inatumai kiwango cha biashara kitafikia dola bilioni 50 katika miaka ijayo.

Matokeo mazuri

Alisema Uturuki imekuwa mshirika wa kimkakati wa Afrika - kutokana na mipango ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ya kuimarisha uhusiano wa Uturuki na Afrika katika miaka 20 iliyopita.

Uturuki inataka kuvutia wawekekezaji wengi zaidi kutoka Afrika  - Photo -TRT Afrika

"Kwa sasa, idadi ya maeneo ambayo shirika la ndege la Uturuki husafiri kwa ndege barani Afrika ni 64. Haya ni maendeleo muhimu sana,'' Akbulut aliongeza.

Hii inachangia kwa kiasi kikubwa usafirishaji wa bidhaa na huduma kati ya nchi za Kiafrika na Uturuki. Ikiwa na Mabalozi 44 barani Afrika, Uturuki pia imeongeza uhusiano wake na bara.

Fursa tofauti

"Uturuki inasimama na watu wa Afrika katika harakati zao za kupata maendeleo zaidi na ustawi, na ndiyo maana uwakilishi wetu wa kidiplomasia uko katika bara zima," Yuksel aliongeza.

Waziri wa biashara na viwanda wa Guinea-Bissau Joao S. Handem Junior aliwataka wawekezaji wa Uturuki kutumia uwezo wa kibiashara wa Afrika hasa katika nchi yake kupitia ushirikiano kwa manufaa ya pande zote akitaja kilimo kama sekta muhimu.

Afrika inazidi kuwa eneo la mkakati la wawekezaji wa Uturuki/ Picha: TRT Afrika

"Tunataka kujifunza jinsi ya kukuza sekta yetu ya kilimo kutoka Uturuki. Guinea Bissau ina ardhi ya kilimo na chanzo chake kikuu cha mapato ni kilimo,” waziri alisema.

Junior pia alisema, nchi yake itaendeleza ushirikiano wake na Uturuki katika sekta zote na akabainisha ‘’uhusiano wa kushinda na kushinda’’ wa Uturuki na bara la Afrika.

Washiriki wengi kutoka Afrika wanahudhuria kongamano la biasharakatika maonyesho hayo Istanbul.

Dkt. Adamu Abdullahi Dabo, mfanyabiashara kutoka Cameroon alielezea furaha yake kutokana na jinsi bara la Afrika linavyozidi kuwa eneo la mkakati la wawekezaji wa Uturuki.

"Tunahitaji kufanya zaidi ili kutumia uwezo bora zaidi wa kibiashara uliopo kati ya Afrika na Uturuki. Afrika ina mengi ya kile Uturuki inachohitaji, pia Afrika inahitaji kujifunza mengi kutoka kwa Uturki kwa maendeleo yake,” aliiambia TRT Afrika.

Kwa upande wake, Balozi wa Libya mjini Ankara Hassan El-Gelaib alibainisha kuwa kwa kuwa na rasilimali nyingi za asili na mtaji wa watu, Afrika inaweza kuwa na mabadiliko ya kimataifa katika siku za usoni.

TRT Afrika