Sinema za drama zilizoonyesha mwanasheria akivalia suti vizuri na mwenye haiba zilimvutia Clarence Hascheley Mamidi kuingia katika tasnia ya mitindo. /Picha: House of Clarence

Na

Firmain Eric Mbadinga

Baadhi ya picha hubaki akilini, zikibadilisha mtazamo wa mtu kuhusu ulimwengu kwa njia ambazo zinabadili maisha.

Kichocheo katika uchaguzi wa taaluma ya Clarence Hascheley Mamidi kilikuwa ni tamthilia za mwanasheria aliyevalia suti nzuri, mwenye ukarimu ambaye hushinda kesi zisizotarajiwa huku akiwa na mtu aliyeacha chuo kikuu kama mwanafunzi wake.

Kulelewa katika mji mkuu wa Gabon unaozingatia mitindo Libreville, Mamadi (Mamidi) hakuwa na ndoto ya kuwa wakili mashuhuri wa kampuni kama Harvey Specter of Suits.

Ilikuwa ni mavazi yake ambayo yalimvutia Clarence.

"Wazo la kuonekana kama yeye (Specter) likawa jambo la kutamanisha," anaiambia TRT Afrika.

"Unaweza kuona dalili hiyo katika mitindo yangu.

"Clarence ni mbunifu wa mitindo. Mtindo wake - mavazi yenye rangi nzito, kwa kawaida na jozi ya suruali zinazokaa vizuri, flana, na koti, mavazi yanayomfanya kutambulika kwa haraka kwenye mitaa ya Libreville.

Chapa yake, House of Clarence, imejijengea umaarufu mkubwa tangu alipozindua jaketi zinazokaa vizuri kwenye mweili karibu miaka miwili iliyopita.

Suti za kubana ni alama ya chapa ya House of Clarence. Picha: House of Clarence

Wateja wanapenda ubunifu wa Clarence kwa kutoa kwa kutoa nguo za kuvutia - suti za kubana zilizotengenezwa na mbunifu.

Anachagua vitambaa ambavyo daima ni vya ubora wa juu kwa bei inayofaa kila wakati.

"Fikra yangu ni kuhimiza uvaaji wa ubora wa hali ya juu ," anasema Clarence.

"Chapa yetu ni ya bei nafuu inayoakisi umaridadi wa kila siku." Kama tovuti ya House of Clarence inavyotangaza, "Dressing to impress is his hobby horse".

Kushawishiwa na TV

Clarence sio mtu pekee aliyefikia kiwango fulani cha mafanikio na hadhi ya mtu Mashuhuri kufuatia taaluma iliyotokana na kile alichokiona kwenye mtandao au TV.

Maneno ya Clarence Mamidi ni, 'unapoamini katika kile unachofanya, mambo yote yanakwenda sawa. /Picha: House of Clarence.

Mnamo mwaka wa 2019, kitivo cha saikolojia na sayansi ya elimu huko UCLouvain, chuo kikuu kikubwa zaidi cha Ubelgiji kinachotumia lugha ya Kifaransa, kilichapisha kipande cha utafiti kinachoonyesha jinsi wahusika wa TV wanaweza kuwa na athari chanya kwa watoto, kama vile kinaweza kuwa na athari mbaya.

Kulingana na utafiti huo, kadiri wanafunzi wa shule za upili katika darasa la 5 na 6 walivyopenda mhusika fulani katika kipindi cha televisheni, ndivyo uwezekano wa wao kujaribu kuonekana kama mtu huyo na hata kuchagua taaluma sawa.

Katika kesi ya Clarence, alivutiwa jinsi mhusika mkuu wa filamu alivyovaa suti alivaa kwa umaridadi ilikuwa ushawishi mkubwa kwa kazi yake.

Baada ya kusomea masuala ya benki na fedha nchini Ghana, aliamua kujikita katika kutimiza ndoto yake ya kuanzisha biashara ya mitindo.

Familia na marafiki wa Clarence, ambao walikuwa wamewazia mustakabali wake akiwa benki, walihitaji muda kuamini. Lakini pale tu walipoona hio ilikua ni ndoto yake, walimuunga mkono afanikiwe.

"Niliangalia wanamitindo waliofanikiwa katika mitindo ya kimataifa na nilijua kuwa maono yangu yangefanya kazi. Kwa hivyo, nilichohitaji kufanya ni kutafuta pesa ili kuanza. Unapoamini katika kile unachofanya, nyota mambo yanakwenda sawa, na wakati mwingi, matokeo ni chanya," anaiambia TRT Afrika.

Leo, kampuni ya 'House of Clarence' ina timu kamili ya wataalamu ambao huboresha ujuzi kila wakati na kuwapa wateja mitindo ya kisasa inayojumuisha vifaa vingi tofauti.

House of Clarence pia huunda vifaa kama vile viatu, tai, mabegi, vito na manukato. /Picha: House of Clarence

"Linapokuja suala la uvaaji wa mitindo, vifaa vyake vina umuhimu mkubwa. Ndio maana kampuni yetu pia inasanifu na kutengeneza tai na viatu. Pia tuna miwani, mabegi, vito na manukato," anasema Clarence.

Roho ya ujasiriamali

Uamuzi wa Clarence wa kukumbatia njia isiyokuwa na uhakika unaokuja na kuanzisha biashara licha ya kuwa na vyeti ambazo zingeweza kumletea kazi zinazolipa vizuri haswa katika nchi yake ya Gabon, ambako ukosefu wa ajira umesalia kuwa juu.

Mnamo 2023, kiwango cha ukosefu wa ajira kati ya vijana kilipanda kwa zaidi ya asilimia 20.

Clarence anaamini kwamba vijana wanahitaji kuzinduka, kuwa na ndoto kubwa, na kufanya chochote kinachohitajika ili kutimiza ndoto zao. Anashukuru kwamba mambo yamemwendea jinsi yalivyo.

"Ninaendelea kufanya kazi na kuzingatia maoni ya wateja wangu huku nikitafuta kuwaridhisha wateja, kuchukua vipimo na kupeleka moja kwa moja majumbani na sehemu za kazi kuwafanyia urahisi," anaiambia TRT Afrika.

Mamidi anatazamia kupanua chapa ya mitindo inayojumuisha mitindo ya wanawake na watoto. /Picha: House of Clarence

"Nilishangazwa sana na kasi ambayo maagizo yalikuja, kwa kuzingatia bei yetu ya juu kwa chapa ya Gabon."

Ubora ni jambo moja ambalo mbunifu mchanga wa mitindo lazima azingatie.

Anapanga kupanua biashara yake kujumuisha mitindo ya wanawake na watoto, ambayo ingemwezesha pia kuajiri watu wengi zaidi.

Clarence, ambaye anavutiwa na mchezaji wa soka wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, anahimiza kila mtu kufanya bidii katika kazi yake.

''Kila mmoja katika sekta yake anaweza kuleta mchango maalum ili kuboresha zaiti nchi yetu nzuri, "anasema.

"Chukua mfano wangu na wa Aubameyang!"

TRT Afrika