Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ameweka wazi nia yake ya kutaka kugombea Urais wa Zanzibar.
Othman Masoud ambae pia ni Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo ataomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama chake katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Iwapo ACT Wazalendo itampitisha kugombea nafasi hiyo, basi hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Othman Masoud amechukua nafasi ya Makamu wa Rais wa Kwanza Zanzibar kutoka kwa mtangulizi wake, Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki 2021.
Chama cha ACT Wazalendo, kimeunda serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) ambapo kwa mujibu wa katiba, ndicho kilichotoa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, huku Makamu wa Pili wa Rais akitoka CCM.