Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC alikata rufaa Jumanne kwa taarifa na ushahidi wa ukatili nchini Sudan, akisema uchunguzi wake unaoendelea "unaonekana kufichua shambulio la kupangwa, la kimfumo na la kina dhidi ya binadamu."
Mwendesha Mashtaka wa ICC, Karim Khan alitoa taarifa ya video baada ya shambulio la Jumapili lililofanywa na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces, RSF, ambalo lililazimisha kufungwa kwa hospitali kuu katika eneo la magharibi mwa Darfur.
Kundi hilo lilifyatua risasi na kupora hospitali ya al-Fasher, kundi la Madaktari wasio na mipaka liliripoti.
Shambulio hilo lilikuja wakati wa RSF, ambalo limekuwa likipigana na jeshi la Sudan kwa mwaka mmoja, lilizidisha nafasi yake ya kutaka kuuteka mji huo, ngome ya mwisho ya sehemu katika eneo linalosambaa la Darfur.
Mapigano ya wiki mbili mwezi Mei ndani na karibu na al-Fasher yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 120.
"Matukio ya kutisha huko Darfur Magharibi, ikiwa ni pamoja na El-Geneina, mwaka wa 2023 ni kati ya vipaumbele vyetu muhimu vya uchunguzi," Khan alisema.
"Aidha, nina wasiwasi mkubwa kuhusu madai ya kuenea kwa uhalifu wa kimataifa unaofanywa katika al-Fasher na maeneo yanayoizunguka."
Mzozo wa Sudan ulianza mwezi Aprili 2023 wakati mvutano mkubwa kati ya viongozi wa jeshi na RSF ulipozuka na kusababisha mapigano katika mji mkuu, Khartoum, na kwengineko nchini humo.
Vita hivyo vimeua zaidi ya watu 14,000 na kujeruhi maelfu ya wengine, huku vikisukuma wakazi wake kwenye ukingo wa njaa.
Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa lilionya pande zinazopigana mwezi uliopita kwamba kuna hatari kubwa ya kuenea kwa njaa na vifo huko Darfur na kwengineko nchini Sudan ikiwa hawataruhusu msaada wa kibinadamu katika eneo hilo.
Vita hivyo pia vilizua mzozo mkubwa zaidi wa uhamiaji duniani kwani zaidi ya watu milioni 10 wamelazimika kukimbia makazi yao, wakiwemo zaidi ya watu milioni 2 waliovuka na kuingia nchi jirani, Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa limesema.
"Ushahidi ambao ofisi yangu umekusanya hadi leo unaonekana kuonyesha madai ya kuaminika, ya mashambulizi dhidi ya raia, yanayorudiwa na yanayoendelea, dhidi ya kambi za wakimbizi wa ndani," alisema.
"Inaonekana kuonyesha kuenea kwa ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia. Inaonekana kufichua mara kwa mara mashambulizi ya makombora ya maeneo ya kiraia, uporaji wa mali na mashambulizi dhidi ya hospitali."
Khan aliongeza, akisisitiza kwamba "alikuwa na wasiwasi hasa na asili ya kikabila ya mashambulizi haya dhidi ya Masalit na jamii nyingine."
Mahakama ya ICC kwa muda mrefu imekuwa ikichunguza ukatili nchini Sudan, kuanzia mzozo wa awali huko Darfur.
Mahakama imetoa pendekezo la kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir kwa tuhuma za mauaji ya halaiki yanayodaiwa kufanywa huko Darfur kati ya 2003-2008.