Mahakama nchini Rwanda yamhukumu mwalimu miaka 20 jela kwa mauaji ya kimbari

Mahakama nchini Rwanda yamhukumu mwalimu miaka 20 jela kwa mauaji ya kimbari

Wenceslas Twagirayezu, amekutwa hatiani kwa ushiriki wake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Baadhi ya washiriki wa kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, maarufu kama "Kwibuka", yaliyofanyika nchini humo Aprili 7, 2024./Picha: Reuters  

Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda imemtia hatiani Wenceslas Twagirayezu, kutokana na kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Watusi nchini Rwanda, miaka 30 iliyopita.

Mahakama hiyo inayoketi mjini Kigali, imeamuru mwalimu huyo kutumikia kifungo cha miaka 20 jela, kutokana na kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, yalioua zaidi ya watu 800,000.

Mwanzoni mwa mwaka 2024, Mahakama Kuu ilimwachia huru Twagirayezu, maamuzi yaliyokatiwa rufaa na upande wa waendesha mashitaka.

Twagirayezu, alikuwa ni mwalimu katika chuo cha Baptiste Gacuba kilichopo katika wilaya ya Rubavu anatuhumiwa kushiriki katika mauaji ya Aprili 7, 8, and 9, mwaka 1994, katika maeneo tofauti ya Gisenyi, yakiwemo Busasamana na Gacamena, ambapo Watusi wengi walipoteza maisha.

Mwaka 2018, Twagirayezu alirudishwa kutoka Denmark baada ya kukamtwa kwake.

TRT Afrika