Mahakama Kuu nchini Kenya imezuia kwa muda mpango uliopendekezwa wa kampuni ya Adani Group kuruhusu uwekezaji katika Uwanja mkuu wa Ndege wa nchi hiyo kwa miaka 30 ili kuupanua.
Katika maombi ya pamoja, Chama cha Wanasheria nchini (LSK), chama kikuu cha mawakili nchini humo, na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC) ziliambia mahakama siku ya Jumatatu kwamba nchi inaweza kujitegemea kukusanya dola bilioni 1.85 zinazohitajika kuboresha uwanja wa ndege katika mji mkuu Nairobi.
LSK na KHRC zilisema madai ya kukodisha kwa miaka 30 kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), kituo kikuu cha usafiri wa anga Afrika Mashariki, haufai, utatishia kazi za watu na ni hatari ya kifedha.
Hati za korti zilizochapishwa na KHRC kwenye tovuti yao ilionyesha kuwa wamedai mipango hiyo ya kampuni ya Adani haitawapa walipa kodi thamani ya pesa,
Kampuni ya Adani, inayoongozwa na bilionea wa India Gautam Adani, mtu wa pili kwa utajiri barani Asia, halijajibu hadharani agizo la mahakama.
mgomo wa wafanyakazi
"Wakati huo huo mahakama imetoa amri ya kuzuia mtu yeyote kutekeleza au kufanyia kazi pendekezo la Adani lililoanzishwa kibinafsi kuhusu JKIA hadi kukamilika kwa kesi mahakamani," Faith Odhiambo mwenyekiti wa LSK alizema katika akaunti yake ya X.
Msemaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Kenya aliambia Reuters: "Hatutatoa maoni yoyote kuhusu masuala yaliyo mahakamani."
Mwezi uliopita, Muungano wa Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga nchini Kenya uliitisha mgomo kuhusu mpango huo uliopendekezwa, ukisema kuwa utasababisha hasara ya kazi na kuleta wafanyakazi wasio Wakenya.
Serikali ya Kenya imesema uwanja huo wa ndege unafanya kazi zaidi ya uwezo wake na unahitaji kufanyiwa ukarabati wa kisasa na wala hauuzwi.
Imesema uamuzi wowote ambao umefanywa kuhusu kuendelea na kile inachokiita ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi unaopendekezwa kuboresha tovuti hiyo.
Ilisema mnamo Julai kwamba toleo la Adani lilikuwa likikaguliwa. Iwapo makubaliano yatakubaliwa, serikali ilisema kutakuwa na ulinzi kuhakikisha maslahi ya taifa ya Kenya yanalindwa.