Mafuriko na maporomoko ya ardhi magharibi mwa Rwanda yamesababisha vifo

Mvua kubwa ilionyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi magharibi mwa Rwanda imesababisha vifo vya takriban watu 95, afisa mkuu wa serikali alisema Jumatano, wakati mamlaka ikitafuta watu wengine waliokwama majumbani mwao.

"Kipaumbele chetu kikuu kwa sasa ni kufikia kila nyumba ambayo imeharibiwa ili kuhakikisha kuwa tunaweza kuokoa mtu yeyote ambaye anaweza kuwa amenaswa," François Habitegeko, gavana wa Jimbo la Magharibi mwa Rwanda, aliambia Reuters

Pia ameongeza kuwa idadi ya waliokufa imefikia 95. Baadhi ya watu walikuwa wameokolewa na kupelekwa hospitalini, alisema, lakini hakusema ni wangapi.

Wilaya zilizoathirika zaidi katika jimbo lake ni Rutsiro, na watu 26 wamekufa, Nyabihu 19, na 18 kila moja Rubavu na Ngororero, aliongeza.

Habitegeko alisema mvua ilianza Jumanne na kuta za Mto Sebeya zilivunjika kingo zake.

“Udongo ulikuwa tayari umelowa kutokana na mvua za siku zilizopita, hali iliyosababisha maporomoko ya ardhi yaliyofunga barabara,” alisema.

Shirika la Hali ya Hewa la Rwanda limetabiri mvua juu ya wastani wa mwezi Mei kwa taifa la Afrika Mashariki.

TRT Afrika na mashirika ya habari