Mafuriko makubwa yalikumba Jimbo la Borno nchini Nigeria mapema Septemba. Picha: AFP

Na

Halima Umar Saleh

Mafuriko yamezidi kuwa jambo la kawaida na la kuangamiza katika sehemu nyingi za dunia, ikiwa ni pamoja na Afrika.

Kuongezeka kwa matukio ya mafuriko kwa kiasi kikubwa kunachangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo yanaakisiwa na misimu inayobadilika badilika na hali mbaya ya hewa kuwa mbaya zaidi kila mwaka.

Kama majanga yote ya asili, mafuriko huathiri mamilioni ya watu ulimwenguni pote kila mwaka, na kusababisha hasara, kuhamisha familia, kuzorota kwa uchumi wa eneo hilo, na kutoa changamoto kwa mikakati ya kujiandaa na ukabilianaji wa serikali na mashirika ya kutoa msaada.

Mwaka huu, mafuriko yameharibu baadhi ya nchi barani Afrika zikiwemo - Nigeria, Niger, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Chad, Guinea, Liberia, na Mali - pamoja na sehemu za Asia na Ulaya ya Kati.

Licha ya ahadi zilizotolewa na serikali, mashirika, na washikadau kukabiliana na changamoto ya mafuriko ya mara kwa mara, hatua za kupunguza mara kwa mara zinaonekana kutotosheleza.

Kwa hivyo, kuna mapungufu gani kwenye mfumo wa kukabiliana na haya maafa na ni vipi yanawezaje kuzuiliwa? Wataalamu wanaamini kuelewa sababu ya mafuriko mahususi kwa jiografia ni muhimu katika kuandaa mikakati ya kukabiliana na athari hiyo, ikiwa sio kuyazuia.

Sababu mbalimbali

Mvua kubwa ambayo inanyesha nje ya mifumo ya misimu inaonekana kama moja ya sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na sababu kuu ya mafuriko katika sehemu nyingi za dunia, ikiwa ni pamoja na nchi zilizoendelea.

Mnamo Septemba 2023, mabwawa mawili yalivunjika nchini Libya, ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa na watu wengi kupoteza  maisha katika jiji la Derna. Picha: Reuters

Mifumo duni wa maji taka katika baadhi ya mikoa, hasa Afrika, pia inachangia mafuriko. Wakati maji ya mvua yakishindwa kupata njia ya kutoka, huelekea kwenye mfumo wa maji taka na kusababisha mafuriko.

Kuharibika kwa mabwawa, pia, husababisha mafuriko makubwa. Utoaji wa maji unaodhibitiwa ni muhimu ili kuzuia mafuriko wakati mabwawa yanajaa kunaponyesha mvua.

Hilo lisipofanyika, mabwawa yatapasuka, na mafuriko makubwa hayawezi kuepukika. Mnamo Septemba 2023, mabwawa mawili yalivunjika nchini Libya, na kusababisha kumwagika kwa mita za ujazo milioni 30 za maji na kusababisha uharibifu mkubwa huku maelfu ya watu wakapoteza maisha yao katika mji wa Derna, ambao una wakazi wapatao 100,000.

Profesa Yusuf Adamu, mtaalamu wa majanga ya asili kutoka Chuo Kikuu cha Bayero huko Kano nchini Nigeria, anasisitiza umuhimu wa kuelewa jinsi majanga haya yanatokea katika maeneo na nyakati tofauti.

"Huenda kuzuia kabisa haitawezekana, lakini kutambua dalili na kuchukua hatua zinazofaa kunaweza kusaidia kupunguza athari zake," anaiambia TRT Afrika.

Adamu anaelezea masomo matatu muhimu ambayo mamlaka lazima ijifunze kutoka kwa matukio ya awali ya mafuriko ili kujiandaa vyema kwa changamoto zijazo.

Ili kupunguza sababu ya mafuriko, wataalam wanasema Mabwawa yanapaswa kufunguliwa mara kwa mara ili kutoa maji na kutenga nafasi ya maji safi. /Picha: Getty

Ufafanuzi wa data

Kupanga kwa ajili ya tukio lolote linalohusishwa na mvua nyingi kunapaswa kuanza wakati ambapo kuna utabiri wa hali ya hewa isiyo ya kawaida.

“Kama Wakala ya Hali ya Hewa nchini Nigeŕia, (NIMET), ukitabiri kiasi cha mvua ambacho kinaweza kutokea au uwezekano wa mafuriko, hiyo ni ishara ya kuchukua hatua mara moja,” anasema Adamu.

"Ni muhimu kwa serikali na jamii kuchukua mifumo ya tahadhari ya hali ya hewa kwa umakini na kushughulikia masuala yaliyopo."

Pia anapendekeza uzingatiaji mkali wa ratiba za ukarabati wa mabwawa.

"Nguvu ya mara kwa mara ya maji inadhoofisha muundo wa bwawa na nanga zake, na kuifanya iwe rahisi kuporomoka ikiwa itazidiwa na nguvu ya maji. Ukaguzi wa mara kwa mara unapaswa kufanywa ili kubaini uimara wa mabwawa na kufanya ukarabati unaohitajika," Adamu anaiambia TRT Afrika.

Mabwawa pia yanapaswa kufunguliwa mara kwa mara ili kutoa maji na kutoa nafasi ya uingiaji maji safi.

Adamu anataja kisa cha Bwawa la Alou katika Jimbo la Maiduguri katika Jimbo la Borno kama mfano wa jinsi ukosefu wa hatua kwa wakati unaweza kusababisha janga kama lile lililokumba eneo hilo wiki iliyopita.

Kusafisha njia ya maji

Jambo moja muhimu katika kuzuia mafuriko mjini na vijijini ni kuelewa kwamba haiwezekani kuzuia maji kabisa.

Mafuriko ya hivi majuzi katika mji wa Maiduguri nchini Nigeria yalisababisha watu 30, na huku watu 400,000 wakihama makazi yao. /Picha: Yerwa NG

"Maji yanapotoka kwenye chanzo yatatafuta njia ya kumwagika. Serikali zitengeneze njia za maji kupita kiasi," anasema Adamu.

Njia za maji zilizoziba na taka zinazotupwa ovyo ovyo mara nyingi huongeza tatizo kuwa kubwa.

"Ni muhimu kwa kila mtu kuwajibika na kuhakikisha njia za maji hazijazibwa," anasema Adamu.

Msomi huyo pia anaangazia umuhimu wa mito na madimbwi katika kupunguza makali ya mafuriko.

Kwa mfano, huko Kano, juhudi zinafanywa kuchimba na kujenga mabwawa. Hii inahakikisha kwamba maji ya ziada hutiririka ndani ya hifadhi yenye nafasi ya kutosha wakati wa mvua nyingi.

Mipango shirikishi

Kulingana na wataalamu, uhamishaji wa watu kutoka maeneo ambayo mafuriko yanakaribia kunahitaji ushirikiano kati ya washikadau, mamlaka, na umma.

"Mifumo ya hadhari ya mapema inapaswa kuwepo ili kuhakikisha uhamisho kwa wakati, kila inapobidi," Adamu anaiambia TRT Afrika.

Njia zilizoteuliwa za uokoaji na mwongozo wa trafiki pia ni muhimu, kama vile kuwa na mpango wa kusaidia watu walio hatarini wakati wa mchakato.

TRT Afrika