Serikali ya Madagascar inaweka msisitizo kwenye kilimo uvuvi. Picha: TRT

Na Firmain Eric Mbadinga

Sisi ni kile tunachokula. Katika ripoti iliyopewa jina la "Sahani, Piramidi, Sayari", Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa linaonesha kuwa kile ambacho watu hutumia na jinsi chakula hicho kinavyozalishwa huathiri sayari kama vile afya ya umma.

Ripoti hiyo inaonesha uhusiano kati ya uzalishaji wa mifumo ya chakula na tabia za kula. Kwa maneno mengine, watu hula kile kinachozalishwa kwa ziada.

Kisiwa hicho cha Afrika Mashariki kimekuwa kikitumia samaki sio tu kama sehemu ya mlo wao, ila kama chanzo cha lishe bora, lakini katika kukuza ufugaji wa samaki kwa kiwango kikubwa, kama mkakati wa kuongeza uzalishaji wa vyakula vya ndani.

Mwaka 2012, wizara ya uvuvi ya Madagascar ilijiwekea malengo ya kuzalisha angalau tani 307,000 za samaki kwa mwaka, kulingana na mfumo wa sera ya bluu.

'"Moja ya malengo mahsusi ya nyaraka hii ilikuwa ni kukidhi mahitaji sanjari na kuongeza uuzwaji wa nje," anasema Hantanirina Rasoamananjara, mkurugenzi katika wizara hiyo anaimbia TRT Afrika.

Ikiwa imeandaliwa mwaka 2015, rasimu hiyo ni hatua muhimu ya kufikia matumizi endelevu ya bahari na vyanzo vingine vya maji. Sera hiyo inaelezea "Uchumi wa Bluu" kama namna ya kutumia vyanzo vya bahari na rasilimali zingine, wakati huo huo kuhifadhi ikolojia na viumbe hai wake.

Serikali ya Madagascar imeshaanza kutekeleza mikakati kadhaa ili kufikia malengo matano kama yalivyoainishwa katika rasimu hiyo, yenye kurandana na masuala ya malengo ya utunzaji wa mazingira.

Uvuvi wa samaki nchini Madagascar inaisaidia nchi hiyo katika ajira, kuboresha lishe na kuondoa umasikini. Picha: TRT Afrika

"Kuna mkakati wa kitaifa wa kuendeleza kilimo uvuvi ulioanza miaka mitatu iliypita na utaendelea mpaka 2030. Kuna mikakati tofauti kwa ajili ya 'Uchumi wa Bluu, hali ya hewa na uwekezaji wa kitaifa. Pia tunazalisha matango na mengineyo," anaelezea Rasoamananjara.

Hatua hizi zinafadhiliwa na wadau tofauti wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) na baadhi ya mataifa ya magharibi.

Mkakati huo umesambaa katika mikoa 11 kati ya 23 ya nchi hiyo, ikiwemo Analamanga, Atsimo Andrefana, Anosy, Androy, Amoron'i Mania, Boeny, Diana, Fitovinany, Ihorombe, Matsiatra Ambony na Sofia.

Mfano wa Ushirika

Katika eneo la Atsinanana, ushirika wa Tilapia de l’Est ulianzishwa mwaka wa 2014 ili kukuza mbinu za usimamizi wa kisayansi kwa ajili ya kuzaliana aina ambazo ziliipa shirika jina lake.

Ni mojawapo ya kanda zinazoibuka za ufugaji wa samaki zinazofanya kazi kama kitovu kilichopangwa cha ufugaji wa samaki katika maeneo tofauti ya Madagaska.

"Ushirika wetu unafanya shughuli zake mashinani na kwa manufaa ya wazalishaji na, kwa kuongeza, watumiaji wetu," Félicité Ahitantsoa, ​​mkurugenzi mkuu wa chama cha ushirika cha tilapia, anaiambia TRT Afrika.

Vitendo huanzia upangaji wa mnyororo wa thamani wa tilapia hadi usaidizi wa kiufundi kwa wazalishaji, ikijumuisha kuwajengea uwezo.

"Pia hujumuisha ufuatiliaji wa kitaalamu na msaada katika kipindi chote cha mzunguko, hadi kutoa kwa mkopo kwa ajili ya pembejeo zinazohitajika na wadau wakati wote wa ufugaji wa samaki. Pia, tunatoa msaada wa kusafirisha pembejeo na mazao kutoka mashambani. Mwisho kabisa ni uuzaji wa tilapia,” anasema Félicité.

Mafunzo ya kilimo uvuvi yametolewa kwa watu 5,600 kama sehemu ya mkakati huo.Picha:/ TRT Afrika

Ushirika huo una matawi manane kwenye mikoa yake, unaoundwa na wazalishaji 500 wakiwemo vijana, wanawake na wavuvi wa jadi.

Mafunzo ya kilimo uvuvi yametolewa kwa watu 5,600 kama sehemu ya mkakati huo.

Kuimarisha Lishe

Msukumo endelevu wa ufugaji wa samaki wa nchi hiyo unaungwa mkono kwa mantiki ya kiuchumi.

Katika vijiji kadhaa vya wilaya ya Amboasary, inayopatikana mkoa wa Anôsy, shirika la Madaktari wasio na mipaka linasema kuwa "wastani wa asilimia 28 ya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano wana utapiamlo, huku robo tatu yao wakiwa katika hali mbaya inayowezesha kusababisha vifo".

Ukweli wa namna hii unaamsha ari ya kuzalisha viumbe vya samaki vinavyopatikana eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya watu na kuuzwa.

"Ufugaji samaki una nafasi kubwa ya kufikia malengo tofauti kama vile lishe, ajira na kuondoa umasikini.Sekta hii inaendana na ardhi na mahitaji yetu. Madagascar ina mito 40 na hekta 150,000 za vyanzo vingine vya maji ambavyo vinafaa kwa ajili ya shughuli ya ufugaji," anasema Rasoamananjara.

Matumizi ya samaki kwa mwananchi mmoja wa Madagascar ni kilo 7, ukilinganisha na kilo 11 barani Afrika. Picha: TRT Afrika

Matumizi ya Samaki kwa mwananchi mmoja wa Madagascar ni kilo 7, ukilinganisha na kilo 11, barani Afrika.

Toka mwaka 2018, uzalishaji wa samaki kwa mwaka umekua na kufikia tani 140,000 kwa aina tofauti za samaki. Mwaka huu, mamlaka za nchi hiyo zimeamua kusambaza samaki 125,000 kwa wazalishaji.

Changamoto za hali ya hewa

Ingawa ufugaji wa samaki unajizoelea umaarufu kama shughuli ya kiuchumi, usumbufu unaosababishwa na hali ya hewa umezidi kuathiri sekta hiyo.

Ukame katika baadhi ya maeneo na vimbunga vikali kwingineko vimekuwa sehemu ya ukweli huu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na kuharibu maisha na kusababisha misukosuko ya kijamii.

Mwanzoni mwa mwaka huu, kimbunga cha Alvaro kiliua watu 19 na kuathiri zaidi ya watu 32,000 katika mkoa wa Fitovinany, unaopatikana kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Mwaka uliofuata, kimbunga cha Freddy kiliua watu 15, na kuharibu makazi 1,000 na kuwaacha wengine zaidi ya 40,000 bila makazi.

Kusini mwa nchi hiyo, ukame umekuwa chanzo cha uharibifu wa hali ya hewa katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

TRT Afrika