Mawaziri wa Utamaduni wa Ufaransa na Madagascar wamechukua hatua ya kwanza ya kurudisha mabaki ya binadamu yaliyochukuliwa kutoka Kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi pindi kilipokuwa chini ya utawala wa Ufaransa.
Alhamisi, kamati ya pamoja ya sayansi ilifanya tathmini, ombi la Madagascar la kuitaka Ufaransa kurudisha fuvu la kichwa cha Mfalme Toera, aliyeuliwa na wanajeshi katika siku za mwanzo za ukoloni.
Tathmini hiyo ni ya mwanzo ya aina yake tangu Ufaransa kupiga kura Disemba 2023 ya kuwezesha urejeshaji wa mabaki ya binadamu yanayohifadhiwa katika taasisi za umma.
"Ufaransa inataka kujibu matarajio haya," Waziri wa Utamaduni Rachida Dati aliwaambia waandishi wa habari, akiwa pamoja na mwenzake wa Madagascar Volamiranty Donna Mara.
Mabaki haya ni "muhimu sana" kwa watu wa Madagascar, amesema Mara.
'Hatua ya mapatano'
Madagascar imetangaza uhuru mwaka 1960 baada ya zaidi ya miaka 60 chini ya utawala wa Ufaransa.
Kamati itatoa maoni yake kwa serikali ya Ufaransa, ambayo baadae itaamua kuyarudisha mabaki ya Mfalme Toera na yale ya machifu wawili kutoka jamii ya Salakava, yote yakiwa yamehifadhiwa katika makumbusho ya historia asili mjini Paris.
Ufaransa imepigia kura sheria kadhaa hivi karibuni zenye lengo la kurudisha katika nchi zake za asili mabaki yanayoshikiliwa katika makumbusho.
Bunge la nchi lilipitisha sheria ya kuwezesha kurudisha kazi za sanaa zilizoibiwa na Nazi kutoka kwa wamiliki wake wa Kiyahudi mwaka huo huo ilipiga kura ya kurudisha mabaki ya binadamu.
"Hii ni hatua ya mapatano," amesema Mbunge Christophe Marion pindi alipowasilisha muswada wa kurudisha mabaki ya kale mwezi November. "
Thuluthi moja ya vitu 30,000 vinavyokadiriwa kushikiliwa katika makumbusho ya Musee de l'Homme, ni mafuvu ya vichwa na mifupa.
Lakini sheria inayoruhusu kurudishwa kwa mali hizo zilizochukuliwa wakati wa ukoloni bado haijafikia hatua za mwisho huku kukiwa na mkwamo kutoka mrengo wa kulia mapema mwaka huu.
"Tunataka tuyarudishe tena haya masuala mezani," Dati amesema, na kuongeza kwamba, "haya ni masuala muhimu" kuponya vidonda vya kihistoria.