Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni ndani ya ikulu ya Kremlin, Machi 20, 2024./Picha: Reuters  

Na Hannan Hussain

Vladimir Putin anaweza kuwa ameshinda Urais kwa mara nyingine, lakini ni jambo lililowazi kuwa msuguano kati ya Urusi na nchi zingine za Magharibi utaendelea kuwepo hata ukawa mbaya zaidi.

Wiki hii, Moscow iliungana na China kupiga kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kusitishwa wa mashambulizi ya Gaza.

Balozi wa Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa Vassily Nebenz aliilaumu Marekani iliyounga mkono azimio hilo, kwa kuleta siasa katika jitihada za kuzitisha mapigano hayo na "kuihadaa jumuiya ya kimataifa."

Katika mahojiano ya hivi karibuni, Pution alionya kuwa Urusi iko tayari kutumia silaha za nyuklia kufuatia vitisho vya mamlaka yaie, ikidai kuwa iko tayari kutumia silaha hizo katika mapambano.

Hii ni mifano ya hivi karibuni ya kuongezeka kwa msuguano kati ya nchi za Magharibi na Moscow.

Mbali na Gaza, kuna vita nchini Ukraine, mojawapo ya viashiria vikubwa vya kushikamana. Wiki hii, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisisitiza mara mbili maoni yake kuhusu kutuma wanajeshi kuiunga mkono Ukraine. Lakini mzozo wa moja kwa moja kati ya Urusi na NATO "ungekuwa hatua moja kutoka kwa Vita vya Kidunia vya Tatu," Putin alionya.

Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz hivi karibuni aliliambia bunge la nchi hiyo kuwa Berlin haitokubali amri ya Putin dhidi juu ya Ukraine.

Umoja wa Ulaya umekubali kuweka vikwazo vipya kwa maafisa na mashirika ya Urusi kufuatia kifo cha mkosoaji mkubwa wa Putin, Alexei Navalny huku wasaidizi wakuu wa kijeshi wa Ukraine huko Magharibi wakiapa kuongeza usambazaji wa silaha.

Shambulizi dhidi la Urusi dhidi ya Ukraine katika kituo cha kuzalisha umeme katika eneo la Kharkiv (SERGEY BOBOK / AFP).

Hata hivyo, Putin amedhamiria kupata ushindi kamili nchini Ukraine, na ameahidi kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Urusi. Pia ameiagiza Huduma ya Usalama ya Shirikisho (FSB) kusaidia kampuni za Urusi katika kuvunja vikwazo vya Magharibi.

Muhula wake wa tano madarakani utampa Putin nguvu ya kiuchumi na fursa ya kiasiasa kutekeleza sera zake, zikiwemo vita nchini Ukraine.

Putin anatarajia kuongezeka udhibiti wa eneo la Urusi juu ya Ukraine, na anajiandaa kuweka eneo maalumu la kuzuia mashambulizi ya kuvuka mpaka. Hii yote ni ishara kwamba Putin hatalegeza msimamo wake katika vita hivyo au kusitisha shinikizo la nchi za Magharibi hivi karibuni.

Eneo la Magharibi inakabiliwa na chaguo dogo juu ya Urusi. Sana sana, msaada wa kijeshi wa Magharibi kwa Kiev unazidi kupungua, na unaonekana kutopendwa na watu wa ndani.

Urusi imeendelea kuishambulia Ukraine./Picha: 

Kulingana na Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov, ahadi ya mataifa ya magharibi kutoa silaha "hazijumuishi uwasilishaji," na karibu nusu ya misaada ya kijeshi imeshindwa kufika nchini kwa wakati.

Hata kama msaada wa Magharibi ungeongezeka kwa kiasi kikubwa, haijulikani ni muda gani hii inaweza kudumu. Usambazaji wa silaha thabiti haujaimarisha ulinzi wa Ukraine hapo awali, na matarajio ya uvamizi uliotafutwa kwa muda mrefu yanaonekana kuwa mbaya zaidi kuliko hapo awali.

Kinyume chake, kuongezeka kwa mpango wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine unaleta mtanziko mgumu kwa nchi za Magharibi: ama kuendelea na vita visivyopendwa na watu wengi, au kulazimisha Kiev kuafikiana kupitia mazungumzo ya amani.

Chaguo la pili linafaa kupewa kipaumbele. Nchi za Magharibi zimepinga matarajio ya mazungumzo ya amani kwa miezi kadhaa, na kutafsiri kama ishara ya kusalimu amri kwa Moscow. Hali hii inaweza kubadilika kwani Putin ataendelea kukaa madarakani hadi 2030.

Donald Trump na Vladimir Putin baada ya Mkutano wao uliofanyika mjini Helsinki nchini Finland, mwaka 2018./Picha:(Reuters/Leonhard Foeger).

Kwa sasa, Washington inaelekea katika uchaguzi ambao unaangazia vipaumbele tofauti vya Ukraine. Ingawa Rais wa Marekani Joe Biden anapenda kuinga mkono Ukraine, mpinzani wake mkuu mwezi Novemba ni Rais wa zamani Donald Trump, ambaye ni mpinzani mkuu wa vita hivyo.

Trump anadai kuwa anaweza kusitisha vita hivyo ndani ya 24, na amekuwa na jukumu muhimu katika kukwamisha mabilioni ya dola katika msaada wa kijeshi kwa Kiev. Huku umaarufu wa Trump ukiongezeka, Putin anaweza kuhisi kulazimishwa kucheza mchezo wa kusubiri huko Ukraine.

Wakati huo huo, Uingereza na Ufaransa zimeonekana na kuchukizwa na uamuzi wa Moscow kuendelea kusogeza vikosi vyake Ukraine.

Kuonekana kwa wanajeshi wa NATO chini kunaweza kuhatarisha mzozo mkubwa zaidi, na Putin ameonya nchi za Magharibi dhidi ya kukiuka safu hii nyekundu. Washirika wa Washington barani Ulaya pia wako chini ya shinikizo la kuzuia mzozo mkubwa wa NATO-Russia.

Kulingana na ripoti ya taasisi ya Study of War, Moscow inajiandaa kwa mapigano ya hali ya juu na NATO. Chanzo cha matayarisho haya ni ongezeko la uwezo wa Urusi kijeshi.

Putin anatazamiwa kusimamia juhudi muhimu za kisasa, ikiwa ni pamoja na kuunda majeshi mawili ya pamoja ifikapo mwisho wa mwaka huu. Mabadiliko ya mbinu ni muhimu kwa nchi za Magharibi kupunguza hasara za kutisha katika uwanja wa vita, kupunguza mvutano wa siku zijazo na Urusi, na kuzuia vita vya Ukraine kutoka nje ya udhibiti.

Hata hivyo, bado kuna uchache wa chaguzi.

Nguvu ya Magharibi juu ya uchumi wa Urusi ina mipaka yake. Putin ana nia ya kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Moscow kutoka mwaka jana, ambayo ilikuja kinyume na maelfu ya vikwazo vya Magharibi.

Muhula wa tano wa kihistoria wa Putin utajaribu uungwaji mkono wa muda mrefu wa nchi za Magharibi kwa Ukraine, kuishinikiza NATO kuibana Urusi, na kufanya iwe vigumu kwa nchi za Magharibi kuweka kando uchumi ambao unawapendelea washirika mahali pengine.

Wakati huo huo, kuongezeka kwa msuguano na nchi za Magharibi kutaimarisha uhusiano wa Moscow na China ambaye ni mshirika mkuu ambaye ameisaidia Urusi kuhimili vikwazo vya Magharibi. Putin anatazamiwa kuzuru Beijing katika safari yake ya kwanza baada ya uchaguzi, na nchi zote mbili zina ya kuwekeza katika maeneo ambayo ushawishi wa jadi wa Magharibi unapungua, kama vile Mashariki ya Kati.

Kwa hiyo, majaribio ya kuitenga Urusi yanaweza kuendeleza ushirikiano wake na nchi zingine ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Uchina, na mshirika mkuu wa Marekani, India. Watatu hao wa mwisho pia ni sehemu ya BRICS, kundi la mataifa yenye uchumi unaoibukia ambayo yanalenga kupunguza utawala wa Marekani katika uchumi wa dunia.

Kwa jumla, muhula wa tano wa kihistoria wa Putin utaweka katika kipimo, uungwaji mkono wa muda mrefu wa Magharibi kwa Ukraine, kuishinikiza NATO kuibana Urusi, na kufanya iwe vigumu kwa nchi za Magharibi kuweka kando uchumi ambao unawapendelea washirika wengine.

TRT Afrika