Utamaduni wa Sapeur ni aina ya kipekee ya mavazi nchini Kongo. /Picha: Picha za Getty

Na Pauline Odhiambo

Iwapo utatembelea mji mkuu wa DRC Kinshasa au jiji jirani la Brazzaville katika Jamhuri ya Kongo, kuna uwezekano mkubwa utapata idadi kubwa ya wanaume au wanawake waliovalia kipekee.

Na kwa mavazi ya kipekee, tunamaanisha mavazi yenye rangi kutoka kichwani hadi miguuni au suti nzuri kutoka kwa brandi maarufu duniani. Na haijalishi ni wapi unatembea au unaendesha gari - kutoka mitaa ya katikati mwa jiji hadi makazi yasiyo rasmi - kwa hakika utaona kundi la watu waliovaa nguo hizo za kuvutia macho.

Ili kuondoa sintofahamu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Kongo ni nchi mbili tofauti. DRC ilikuwa chini ya ukoloni wa Ubelgiji, huku ya Jamhuri ya Kongo ilikuwa chini ya ukoloni Wafaransa.

Mji mkuu wa DRC ni Kinshasa na mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo ni Brazzaville.

Ukweli mwingine wa kuvutia ni kwamba miji mikuu miwili imetenganishwa na eneo la kilomita 7 la Mto Kongo.

Wanahistoria wanafuatilia uvaaji wa kipekee wa watu wa Kongo hadi miaka ya 1920, wakati mataifa yote mawili ya Kongo yalikuwa chini ya utawala wa kigeni.

Wakati baadhi za jamii ziliungana na upinzani ulioratibiwa dhidi ya watawala wa kigeni, kikundi fulani - huko Kinshasa na Brazzaville - kiliamua kuvaa kama watawala wa kikoloni.

Vazi la kipekee la watu wa Kongo lilianza miaka ya 1920 wakati mataifa yote mawili ya Kongo yalikuwa chini ya utawala wa kigeni. /Picha: Getty

Na kundi hili la watu hawakuwa watu wa Kongo wa kawaida, bali watumishi walioajiriwa na raia wa Ubelgiji na Ufaransa.

Kuweka wazi, ilikuwa zaidi ya "ndiyo, wewe ni bosi, lakini ninaweza kuvaa, na kutenda kama wewe."

Watumishi hao walikusanya malipo yao kidogo ili kununua nguo za nchi za magharibi, huku baadhi yao, ambao waliwekwa kazini Ubelgiji au Ufaransa, walirudi Kongo na nguo walizopewa na mabwana zao.

"Sape inamaanisha jamii ya wapenda mazingira na watu wa kifahari," anasema mtumiaji wa TikTok St Germain de Londres.

Kwa Kifaransa, ambianceurs ni watu wanaotumbuiza umati kwenye karamu au mkusanyiko wa watu.

"Wengine huwa wanavaa jaketi nene za msimu wa baridi na buti za msimu wa baridi katika nchi au bara ambapo koti nene za msimu wa baridi na buti za msimu wa baridi hazihitajiki," asema mtumiaji mwingine wa Tiktok.

Wanahistoria wameandika kwamba kuvaa mavazi ya kifahari ilikuwa aina ya ujanja ya uharakati wa watu wa Kongo. Miaka iliposonga, uvaaji huo mkali ulipata umaarufu miongoni mwa makundi mbalimbali ya jamii ya Kongo.

Ubunifu pia ulichukuliwa kuwa wa hali ya juu zaidi, huku baadhi ya watu wa Kongo wakichanganya sehemu ya mavazi ya kitamaduni na mavazi ya kisasa wa Kizungu, mchanganyiko ambao ulitokeza kile kinachojulikana leo kama "utamaduni wa Sapeur." Watu wa Kongo wanaiita La Sape kumaanisha "uvaaji wa hali ya juu."

Ingawa haijaandikwa, utamaduni wa kuvaa unawakilisha kujieleza, utamaduni na upekee. Na upekee huu unaweza kuja kwa namna ya kofia za fedora zenye kung'aa, bakora ndefu nzuri, kukata mkato wa nywele wa kuvutia, suti za rangi, viatu vya ngozi ya mamba, na nguo za wabunifu.

Mtindo wa Sapeur unawakilisha kujieleza, utamaduni na upekee. /Picha: Reuters

La kushangaza ni ya kuwa 'sapeur' anaweza kuishi katika nyumba ambayo kodi yake ya kila mwezi ni dola 50 za Marekani, lakini huweka akiba na mara kwa mara hununua nguo na viatu vya wabunifu vya bei ni zaidi ya dola 300 za Marekani.

"Hao ma 'sapeur' wanapaswa kuwekeza pesa zao badala ya kuzipoteza kwenye nguo za wabunifu," anasema M. G Evie kwenye Tiktok.

Lakini 'sapeurs' wengi wanasema lengo la kufanya hivo ni rahisi: lengo ni kuwa ishara ya ukaidi kwenye nysuo zenye shida.

Wengine wanasema, ni mazoea, na kuacha utamaduni ni ngumu.

Gharama wanayotoa kwa mavazi ya kifahari na sura nzuri ni pesa zinazotumika vizuri.

Mwanamuziki wa Rhumba wa Kongo marehemu Papa Wemba anasifika sana kwa kueneza utamaduni wa 'La Sape'. Kwa kweli, aliwahi kusema 'La Sape; ni kama dini.

Papa Wemba alipewa jina la utani "le Pape de La Sape" kumaanisha "baba wa sapeurs".

TRT Afrika