Kufichua mishahara ya viongozi kunaonekana kama ishara ya uwazi serikalini. Picha: Nyingine

Na Firmain Éric Mbadinga

Udadisi wa umma kuhusu mishahara kwa ujumla, na mishahara ya watu mashuhuri haswa, umezua majukwaa mazima mtandaoni yanayolenga kujibu swali ambalo kidesturi mtu hatakiwi kuuliza moja kwa moja.

Ikiwa kweli "kazi zote zinastahili mshahara wa aina fulani'' hakika malipo ambayo Rais wa nchi anayo haki hayawezi kuepukwa katika uchunguzi kama huo. lakini sio barani Afrika, angalau, ambapo mishahara ya viongozi haifichuliwi mara nyingi.

Kufichuliwa kwa malipo ya rais na maoni ya umma kuhusu hili vinaonekana kama ishara ya uwazi na utawala bora.

Kwa kuzingatia asili ya tawala maalum katika nchi nyingi za Kiafrika, hitaji la uwazi linaweza kuwa haliwezekani kila wakati. Katika hali nyingi, utamaduni wa kuficha siri za serikali usio rasmi huzima maswali kama vile mapato ya mkuu wa nchi - isipokuwa kama kuna ufichuzi wa hiari.

Katika nchi nyingi, hakuna sheria zinazowaamuru viongozi kufichua mishahara yao. Picha: AFP

Nchini Gabon, kwa mfano, tangazo la kiongozi wa junta Brice Oligui Nguema la Oktoba 18 kuhusu kukataa mshahara wake wakati wa kipindi cha mpito nchini humo limeibua upya udadisi kuhusu malipo ya urais.

Takwimu zisizoeleweka

Joëlle Samia Samogho, mhitimu wa sayansi ya siasa anayeishi Libreville, anaamini kuwa ni mwiko kuuliza Rais wa nchi hiyo analipwa nini.

"Utagonga mwamba ukifuatilia suala hili. Katika nchi yetu, inaonekana kutaka kujua ni kiasi gani mkuu wa familia anapata. Kwa vyovyote vile, habari nadra sana kupata habari zozote kuhusiana na hili," anaiambia TRT Afrika.

Jacques Matand, mwandishi wa habari wa Kongo, anakubali. "Swali lolote linalohusiana na mshahara wa Rais linatawaliwa na aina fulani yas sheria ya ukimya)," anasema.

Ingawa taarifa chache zinapatikana kwa ujumla, jarida la Business Insider Africa, ambalo linajishughulisha na masuala ya fedha, ilizindua orodha ya "Marais 5 bora wa Afrika wanaolipwa vizuri zaidi" mnamo Agosti 2022.

Marais wenye mishahara mikubwa zaidi Afrika

1. Rais Paul Biya wa Cameroon - US $ 620,976 kwa mwaka.

2. Mfalme wa Morocco - $ 488,604 kwa mwaka.

3. Yoweri Museveni wa Uganda - $183,216 kwa mwaka.

4. Rais Akufo Addo wa Ghana - $ 74 000 kwa mwaka.

Nchini Senegal, Rais Sall, ambaye amesalia na miezi michache tu madarakani baada ya kutangaza kutogombea tena muhula mpya, alitangaza mwezi Aprili 2017 kwamba alikuwa ametoa amri ya kuweka kiwango cha juu zaidi cha mishahara yote kuwa Faranga milioni 5 za CFA. ($ 8 400) kwa mwezi.

Kama Senegal, baadhi ya nchi za Afrika zinajaribu kufafanua mshahara maalum kwa Marais wao na kuweka masharti ya uwazi.

Nchini Gabon, ripoti iliyoandaliwa mwaka 2018 na Mays Mouissi, mchambuzi wa uchumi wa Ufaransa na Gabon ambaye sasa anaongoza wizara ya uchumi, inaonyesha kwamba "katika hali ya jumla, waziri wa nchi anapokea wastani wa faranga za CFA milioni 6.5 kwa mwezi".

Mawaziri wa nchi pia wana haki ya marupurupu ya safari za kikazi wanaposafiri ndani ya Gabon na nje ya nchi.

Dk Balla Doumbia, mwalimu na mtafiti mwenye shahada ya udaktari katika sosholojia inayozingatia sheria, anashikilia kuwa tofauti ya mtazamo wa mishahara ya marais wa Afrika ni kwa sababu "katika katiba nyingi, mshahara wa mkuu wa nchi haujafafanuliwa".

"Ili kujua ni kiasi gani mkuu wa nchi anapata, unapaswa kuangalia mfumo wa kisheria," Dk Doumbia anaiambia TRT Afrika.

"Rais anachukuliwa kuwa taasisi. Katika hali hiyo, ili kujua mshahara wa Rais ni upi, tunapoandaa bajeti ya Serikali, tunazingatia vipengele vyote vinavyounda utumishi wa Rais wa Jamhuri."

Nigeria, nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika, ilitengeneza upya sarafu yake mnamo Februari 2023. Picha: Others

Hii ina maana kwamba hakuna mswada wa fedha ulio na sura yoyote iliyotolewa kwa mkuu wa nchi.

“Tutachokiona ni posho tu, miaka ya 1960 baada ya uhuru wakuu wa nchi walipewa mamlaka kadhaa ambayo hayakuwekwa wazi, kwa upande wa siasa, kwa mfano, uliundwa ‘mfuko maalum’ ili kumuwezesha mkuu huyo kumudu gharama ya serikali kuzuia vitisho vya kigeni, na wakati huo, hii ilikuwa sehemu ya mshahara wa mkuu wa nchi," anaelezea Dk Doumbia.

Anatoa mfano wa Mali, ambapo wakuu wa nchi walikuwa wakilipwa mishahara mikubwa kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyoainishwa kama "siri za serikali".

''Pamoja na ujio wa demokrasia nchini Mali mwaka 1992, tulilazimika kutatua mambo. Huduma hizo zilizoainishwa kama siri za serikali, ikiwa ni pamoja na huduma za usalama, zilipaswa kutengwa na usimamizi wa moja kwa moja wa mkuu wa nchi, "anasema Dk Doumbia.

Kulingana na mwalimu-mtafiti, Sheria ya Fedha, kwa kuzingatia sheria asili ya nchi, huratibu mshahara wa mkuu wa nchi. Kifungu hiki lazima kwanza kichunguzwe na Mahakama ya Kikatiba, ambayo itatathmini upatanifu wake na Katiba.

"Ikiwa sheria ya asili ya urais inapendekeza mafao au posho ambazo zimetiwa chumvi na ambazo zinaweza kuhatarisha matumizi ya umma, sheria hii inaweza kubatilishwa," anasema Dk Doumbia.

Kulingana na nchi na mashirika yake ya ndani, utaratibu wa kufafanua mshahara wa rais unaweza kutofautiana na, wakati mwingine, kuwekwa mbali na umma, na kuimarisha tafsiri mbalimbali, iwe na msingi au la.

TRT Afrika