Mtazamo huo una mizizi yake tangu enzi za ukoloni na fikra za walowezi wa kikoloni. Kwa hivyo, badala ya kuchukulia masuala ya Afrika kwa uzito unaostahili, mara nyingi bara la Afrika huangaliwa kupitia lenzi ya maslahi ya nchi nyingine.
Lakini hebu tufafanue jambo moja vizuri: hatuzungumzii juu ya bara ambalo kila kitu kinafanana. Bara hili ni mchanganyiko wa mifumo tofauti ya kisiasa, lugha, makabila na tamaduni.
Hata hivyo, ni wakati wa kutambua mtazamo wenye nguvu ambao kimsingi umelenga kushusha thamani ya bara la Afrika. Pengine tayari unazifahamu kauli kama hizi: "Uwekezaji wa nchi X barani Afrika unaongezeka" au "Afrika yageuka uwanja mpya wa vita kwa mataifa makubwa A na B".
Hata hivyo, ni wakati wa kutambua mtazamo wenye nguvu ambao kimsingi umelenga kushusha thamani ya bara la Afrika. Pengine tayari unazifahamu kauli kama hizi: "Uwekezaji wa nchi X barani Afrika unaongezeka" au "Afrika yageuka uwanja mpya wa vita kwa mataifa makubwa A na B".
Katika hilo, masuala matatu muhimu yanajitokeza zaidi, yakifichua kwa nini mijadala kuhusu Afrika imechukua mkondo huo.
Lugha kama Kielelezo cha Mahusiano ya Kitabaka
Mazungumzo kuhusu Afrika si suala la maneno tu, bali linagusia nani mwenye nguvu. Lugha tunayotumia inaakisi nani ameshika mpini, na kwa bahati mbaya, kushushwa kwa thamani ya utu wa Afrika ni sumu inayoendelea kutoka enzi ya ukoloni.
Lugha ina nguvu. Inaweza kubadilisha mwendo wa historia kulingana na istilahi zilizotumika. Katika Afrika, kuwekwa kwa lugha za Ulaya kama lugha rasmi wakati wa ukoloni kuliharibu jinsi bara hilo lilivyochukuliwa na kusawiriwa.
Ilifanya kazi kama chombo kilichosambaza mtazamo, fikra na uandishi wa Ulaya kuhusu Afrika, zikiendeleza masimulizi ya kudunisha na ya kigeni. Kimsingi, ukoloni ndio chanzo cha kudunishwa kwa Afrika. Na kwa sababu hiyo, jinsi tunavyozungumza, kuandika, na kujadili Afrika leo bado kunaonyesha urithi wa hii sumu.
Mchango wa Itakadi ya Uliberali
Nadharia za mahusiano ya kijamii zilizoletwa na uliberali zililenga dhana mahususi ambayo iliwatenga watu weusi kushiriki katika mifumo ya kiserikali na makundi ya kiraia.
Hali ya hewa ya kibaguzi katika kile knachoiitwa Kustaarabika kwa Ulaya iliweka dhana ya ushirikishwaji pembeni. Kama ilivyobainika, "Mkataba wa Kijamii" halikuwa jina sahihi kutumika - kama vile alivyoandika mwandishi Charles W. Mills katika kitabu chake "Racial Contract".
Katika muktadha huu wa kinadharia, haishangazi kwamba kikundi kinachochukuliwa kuwa "hakikustaarabika" kimegeuzwa kama kitu kinachohitaji kufanyiwa marekebisho na wale "walioshaarabika". Mtazamo huu sio mpya na umejidhihirisha kwa njia tofauti katika historia.
Mbinu inayojulikana kama "uliberali wa kisasa" ambayo ilitumiwa kuendeleza sera ya kigeni ya Marekani kufuatia Vita Baridi, ni mfano wa kushangaza wa udanganyifu wa kudai kuleta "uhuru" kwa kanda"zisizo huru".
Mbinu inayojulikana kama "uliberali wa kisasa" ambayo ilitumiwa kuendeleza sera ya kigeni ya Marekani kufuatia Vita Baridi, ni mfano wa kushangaza wa udanganyifu wa kudai kuleta "uhuru" kwa kanda"zisizo huru".
Mbinu hizi zinasisitiza upendeleo wa asili uliopo katika kufafanua ni nani "mstaarabu" na hilo linatoa umuhimu wa kuhoji na kupinga mitazamo finyu kama hio.
Mwendelezo wa uharibifu wa Uliberali Mamboleo
Uliberali mamboleo ulikuja kwetu chini ya kivuli cha utandawazi na kuondoa kile Wendy Brown alichoita "mapinduzi ya chini kwa chini."
Mfumo huu mpya wa kiuchumi umeyaguza maisha ya binadamu kuwa bidhaa au mali ambayo huthminishwa kulingana na faida za kifedha.
Wakati huo huo, mamlaka za wakoloni wa kale zilifanya uhandisi wao wa kijamii kwa njia ya misaada ya maendeleo, kuendeleza tofauti kati ya bwana na mtwana. Na katika Afrika, udhalilishaji huu ulichukua sura ya kificho zaidi.
Rais Macron aliwahi kufichua ubaya wa utegemezi wa misaada, nafasi ya uongozi, na mtazamo unaozingatia ustaarabu, katika hotuba yake kwa Mataifa ya viwanda (G20) mwaka 2017: "Mpango wa Marshall ulikuwa mpango wa ujenzi […] Changamoto ya Afrika ni tofauti kabisa na kubwa zaidi, ni ya ustaarabu wa leo. ,” alisema Macron, akiongeza kwamba “tunahitaji kuendeleza sera ambazo ni za kisasa zaidi kuliko Mpango wa Marshall.”
Katika hotuba yake, aliwanyooshea kidole wanawake wa Kiafrika, akidai kuwa kuzaa watoto saba au wanane ndiyo chanzo cha kukosekana kwa utulivu barani Afrika. Mchezo huu wa lawama ni mojawapo ya mifano ya kutatanisha ya jinsi wanawake wanavyowajibishwa kukwamisha maendeleo na maendeleo.
Cha kusikitisha ni kwamba, mtazamo huu si jambo geni katika ulimwengu wa uliberali mamboleo, ambapo maisha ya mwanadamu yanaonekana kuwa ni mtaji tu unaopaswa kutolewa mhanga ili kufikia malengo ya kimaendeleo. Chini ya kivuli cha utandawazi, uliberali mamboleo umebadilisha mbinu za ukoloni wa zamani kwa mng'ao mpya na kuziweka kama msaada wa maendeleo baada ya ukoloni wa kale.
Lakini matamshi haya yanatumiwa kuidhalilisha Afrika na wale wanaodai "kuirekebisha".
TRT Afrika: Afrika, kama ilivyo
Hadithi ya Afrika kama kitu badala ya watu wanaojielewa na kujitegemea ni hadithi isiyo na maana na isiyojificha.
Kwa upande mmoja, ni suala tata lililojikita kutokana na sababu za kihistoria na wa kinadharia ambazo huwatenga watu weusi. Kwa upande mwingine, kusudi lake halijifichi: kutaka kudhibiti juu ya eneo kubwa na tofauti kwa gharama yoyote.
Kwa kugha nyingini, huu ni mwendelezo wa kuimba wimbo uleule kwa mapigo tofauti. Ni wakati wa kusonga mbele, kuachana wimbo wa kale na kutengeneza kuongea masimulizi mapya kuhusu Afrika.
Ni wakati wa kutambua historia yake yenye utajiri, tamaduni mbalimbali, kuiona si kama kitu bali kama watu wenye sauti na hadithi ya kusimuliwa. Hivyo: TRT World imeanzisha TRT Afrika, kutangaza katika lugha 4: Kiswahili, Kiingereza, Kihausa, na Kifaransa.
Hatua kama hiyo inalenga kubadilisha simulizi zilizotawala kote barani Afrika na kuzingatia simulizi muhimu za kimataifa ambazo zinalenga kuonyesha urithi wao wa kijamii, kisiasa na kitamaduni.