Rais wa Gabon Jenerali Brice Oligui Nguema aliapishwa siku tano baada ya mapinduzi yaliyomuingiza madarakani. Picha Reuters

Kiongozi wa mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais wa Gabon Ali Bongo aliapishwa kama rais wa mpito na majaji wa mahakama ya kikatiba siku ya Jumatatu katika hafla ya televisheni iliyoandaliwa ili kuimarisha utawala wa serikali.

Maafisa wa kijeshi wakiongozwa na Jenerali Brice Oligui Nguema walichukua mamlaka mnamo Jumatano dakika chache tu baada ya tangazo kwamba Bongo amepata muhula wa tatu katika uchaguzi - matokeo waliyobatilisha wakisema hayakuwa ya kuaminika.

Nguema alipokelewa kwa shangwe na hadhara ya maofisa wa kijeshi na viongozi alipowasili kwa ajili ya sherehe hizo, na tena mara tu baada ya kuapishwa. Televisheni ya Taifa ilionyesha picha za umati wa watu wenye furaha na vifaru vikifyatulia risasi baharini kuashiria tukio hilo.

Mapinduzi hayo, ambayo yalimaliza miaka 56 ya familia ya Bongo madarakani katika nchi hiyo inayozalisha mafuta, yalivuta umati wa watu waliokuwa wakishangilia katika mitaa ya mji mkuu Libreville lakini kulaaniwa kutoka nje ya nchi.

Viongozi wa jumuiya ya kanda ya Afrika ya Kati ECCAS wanatazamiwa kukutana ana kwa ana siku ya Jumatatu ili kujadili majibu yao kuhusu kuondolewa madarakani.

Wiki iliyopita waliwataka washirika wakiongozwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuunga mkono kurejea kwa haraka kwa utaratibu wa kikatiba.

Junta bado haijasema inatarajia kushika madaraka kwa muda gani. Siku ya Ijumaa, Nguema alisema itaendelea "haraka lakini kwa hakika," lakini akaonya kuwa haraka kupita kiasi kunaweza kusababisha uchaguzi ambao hauna uaminifu.

Reuters