Wabunge walipitisha kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 hadi katikati ya Desemba. / Picha: AA

Vyama vya upinzani nchini Senegal vimeazimia kuandaa maandamano kupinga hatua ya Rais Macky Sall kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 25.

Maamuzi hayo tata yanampa fursa Rais Sall ambaye, muhula wake wa pili ulipaswa kumalizika mapema Aprili, kuendelea kukaa madarakani, pengine mpaka.

Jumuiya ya ECOWAS, Umoja wa Ulaya na Marekani zote zimeitaka Senegal kuendelea kutumia ratiba zake za kawaida za uchaguzi.

Rais Sall alisema Jumamosi kwamba alifikia maamuzi hayo kufuatia mzozo kati ya bunge la kitaifa na Baraza la katiba juu ya kukataliwa kwa wagombea na hofu ya kusababisha machafuko kama yalivyojitokeza mwaka 2021 na 2023.

Takriban mashirika 40 ya kiraia, yakiwemo pamoja na vyama kadhaa vya wafanyakazi, wameungana pamoja kuitisha "siku ya kutochukua hatua" ijumaa katika Mji mkuu Dakar.

Sall ameliambia Baraza la Mawaziri la nchi hiyo kuanza kwa "mchakato wa kutuliza na upatanisho".

Sall alisisitiza uamuzi wake wa kutoshiriki katika uchaguzi na "kuimarisha imani yake kwa Waziri Mkuu Amadou Ba".

Licha ya hayo, upinzani unashuku kuwa ucheleweshaji huo ni sehemu ya mpango wa kambi ya Rais ili kuepuka kushindwa, au hata kuongeza muda Wa Sall madarakani, licha ya yeye kusisitiza mara kwa mara kwamba hayuko tayari kugombea tena.

AFP