Kenya ndio kinara wa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki./Picha: Getty

Kenya inaoongoza kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji, kulingana na ripoti ya hivi karibuni.

Ripoti hiyo iliyotolewa na taasisi ya fedha ya RMB ya Afrika Kusini, inaiweka Kenya katika nafasi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku ikishika nafasi ya 11 barani Afrika baada ya kupata alama 0.14.

Ripoti hiyo, iliyopewa jina la 'Where to Invest in Africa', inatoa picha halisi ya mazingira ya uwekezaji ya nchi 31 Afrika, na namna mataifa hayo yanalivyofanya katika kuweka mazingira bora na thabiti ya uwekezaji.

Pia, inatoa ushauri wa namna gazi sera zinaweza kutumika katika kuboresha utendakazi wa siku za usoni wa nchi na kuvutia uwekezaji.

"Ni matumaini yetu kuwa wawekezaji watatumia utafiti huu kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza mtaji sehemu fulani," anasema Isaah Mhlanga, mchumi mwandamizi kutoka RMB.

Tanzania inashika nafasi ya pili, kulingana na utafiti huo ikiwa na alama 0.12, na ni ya 12 barani Afrika.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam ambao ni kitovu cha biashara nchini Tanzania./Picha: Getty

Rwanda iko katika nafasi ya tatu na 15 mtawalia, ikiwa imevuna alama 0.06, wakati Uganda ikiwa ya nne na ya 19 kwa alama -0.07 wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni ya tano, kwa alama -0.28.

TRT Afrika