Kanali Mike Mikombe Kalamba amekutwa na hatiua ya mauaji.  Wakili wake, Serge Lukanga, alisema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo. / Picha : Reuters 

Kanali wa Kongo amepatikana na hatia ya mauaji na uhalifu mwingine unaohusiana na mauaji ya mwezi Agosti ya watu 56 wakati wa operesheni ya jeshi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakipinga uwepo wa UN Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mahakama ya ndani ilisema Jumatatu.

Kanali Mike Mikombe, ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha Walinzi wa taifa katika jiji la Goma, ambako tukio hilo lilitokea, alikuwa mmoja wa askari sita waliokuwa wakishtakiwa.

Alihukumiwa kifo, lakini hukumu ya kifo haitumiki tena nchini Kongo, na kwa ujumla inabadilishwa kuwa kifungo cha maisha.

Wanajeshi wengine watatu walihukumiwa kifungo cha miaka 10. Naibu wa Mikombe na askari mwingine waliachiwa huru.

Maandamano ya kupinga kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo, MONUSCO mnamo Julai 2022 yalisababisha vifo vya zaidi ya 15, wakiwemo wanajeshi watatu wa kulinda amani huko Goma na mji wa Butembo.

Ujumbe huo wa MONUSCO Mashariki mwa Congo, umekabiliwa na maandamano tangu mwaka jana, yaliyochochewa kwa kiasi na malalamiko kwamba umeshindwa kuwalinda raia dhidi ya miongo kadhaa ya ghasia za wanamgambo.

Wakili wake, Serge Lukanga, alisema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

TRT Afrika na mashirika ya habari
Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuziSera ya Vidakuzi
Kubali