Zaidi ya malori 700 yanayobeba msaada wa chakula wa WFP kwa sasa yanaelekea katika jamii kote nchini Sudan. / Picha: Reuters

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) siku ya Jumanne lilisema kuwa lori zake za chakula ziliwasili katika kambi ya Zamzam Kaskazini mwa Darfur Ijumaa iliyopita, ambako njaa ilithibitishwa mapema mwaka huu, na kuashiria utoaji wa kwanza katika muda mrefu.

"Hizi ni bidhaa za kwanza za chakula za WFP ambazo tumeweza kusafirisha hadi kambini kwa miezi mingi, zikiwa zimebeba msaada wa dharura wa chakula kwa watu 12,500," msemaji wa shirika la chakula la Umoja wa Mataifa Leni Kinzli aliambia mkutano na waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

"Wakati kiasi cha misaada kwenye msafara huu ni tone tu baharini ukilinganisha na hitaji, malori haya yanatoa matumaini kwa watu wa Zamzam ambao wamekuwa wakipambana na njaa peke yao, kukatishwa misaada kwa miezi mingi," Kinzli alisema.

Alibainisha kuwa zaidi ya malori 700 yanayobeba msaada wa chakula wa WFP kwa sasa yanaelekea kwenye jamii kote Sudan.

Wito wa kifungua njia salama za misaada

"Hii ni pamoja na maeneo 14 ambayo ama yanakabiliwa na njaa au hatari ya njaa na ni sehemu ya juhudi za kuongeza mamilioni ya watu katika maeneo yenye uhitaji mkubwa na yaliyotengwa nchini," alisema.

"Kwa jumla, malori hayo yatabeba takriban tani 17,500 za msaada wa chakula, kiasi cha kutosha kulisha watu milioni 1.5 kwa mwezi mmoja."

Alizitaka pande zote kwenye mzozo, wanamgambo na vikundi vyenye silaha au makabila, kuruhusu misafara hii kupita salama, akisisitiza umuhimu wa kupita salama na ufikiaji usio na kizuizi wa kukomesha njaa huko Zamzam na kuizuia kuenea katika maeneo mengine.

Kulingana na msemaji huyo, tangu Septemba, WFP imepeleka msaada wa chakula kwa wastani wa watu milioni 2 kila mwezi kote Sudan.

Maelfu waliuawa katika vita

Tangu katikati ya mwezi Aprili mwaka jana, jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wamekuwa wakishiriki katika mzozo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya 20,000 na kuwakimbia karibu watu milioni 10, kulingana na UN.

Kumekuwa na ongezeko la wito kutoka kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kutaka kumaliza mzozo huo, kwani vita hivyo vimewasukuma mamilioni ya Wasudan kwenye ukingo wa njaa na vifo kutokana na uhaba wa chakula, huku mapigano hayo yakienea katika majimbo 13 kati ya 18 ya Sudan.

TRT Afrika