Ubunifu wa Alassane tayari umeleta nafuu katika jamii. /Picha: Alassane Thiam

Na Firmain Eric Mbadinga

Alassane Thiam, mfua chuma aliyeacha shule ya upili, hakuweza kupoteza wakati wake kufikiria kama shida ya kifedha ingemlazimisha kukatisha masomo yake.

Badala yake, kijana huyu mzaliwa wa Mbar, kutoka jamii moja katika eneo la Fatick magharibi-kati mwa Senegali, alichagua kuelekeza ustadi wake katika uvumbuzi ambao umebadilisha jinsi watu wa maeneo ya vijijini wanavyotumia mafuta kwa kupikia.

Jiko la mafuta taka la Alassane, ambalo ni la matumizi ya kawaida kwa kuwa ni la kipekee, linatokana na kutumia rasilimali inayopatikana kwa urahisi - mafuta ya kulainisha magari yaliyotupwa - kuunda suluhisho la bei nafuu na la ufanisi la kupikia kwa jamii za vijijini.

Ubunifu wake tayari unaonekana kubadilisha jinsi watu wanavyotumia mafuta ya kupikia katika jumuiya ambapo nishati za jadi za jikoni, kama vile kuni na gesi, ni adimu au ni ghali.

Huko Mbar, jiko la Alassane limefaidi takriban wakazi 26,000 ambao baadhi yao ni wafugaji na wakulima wanaoishi katika maeneo yaliokumbwa na ukame.

Jiko linafanya kazi kutumia mashine ya propela. /Picha: Alassane Thiam

"Ninahisi fahari nikifikiria kuwa kile nilichobuni kinawezesha watu kuweka akiba kubwa kwenye mafuta ya kupikia. Hiyo ndiyo zawadi kubwa," anaiambia TRT Afrika.

Rahisi kutumia

Jiko lina sehemu ya kutoa moshi na hifadhi iliyojengewa ndani ambayo huhifadhi mafuta taka, kwa kawaida ni mafuta ya ulainishaji wa gari inayokusanywa kutoka kwa gereji kwa gharama ndogo au bila malipo yoyote.

Jiko linatumia mashine ya propela. Mfumo huo unasukuma hewa ndani, kuweka moto thabiti. Kuna bomba mbili - moja huzungusha mafuta, na nyingine inawezesha kutoa hewa.

Ili kuendesha jiko, watumiaji wanahitaji kuwasha moto na kuzungusha kibomba cha kuwasha, kuhakikisha mtiririko wa hewa na mafuta unaoendelea kwa uthabiti.

Kwa upande wa utendaji, mpangilio huo unalinganishwa na majiko ya kitamaduni, ingawa kwa gharama iliyopunguzwa sana kuliko gesi ya kupikia, kuni au umeme."

Ninahisi fahari nikifikiria kuwa kile nilichobuni kinawezesha watu kuweka akiba kubwa kwenye mafuta ya kupikia. Hiyo ndiyo zawadi kubwa," anaiambia TRT Afrika.

Mfumo wa gharama nafuu

Alassane alibuni jiko la mafuta taka na kuunda jiko hilo kwa mara ya kwanza katika warsha ya baba yake ya ufuaji chuma, akichochewa na wazo la kuunda kitu ambacho kingenufaisha jamii yake na kinaweza kupunguzwa.

"Wazo hili lilitokana na nia yangu ya kuwarahisishia maisha mama zetu ambao mara nyingi wanatatizika kutafuta mafuta ya kupikia, katika jamii yangu ni vigumu kwao kupata kuni, huku gesi ya kupikia ikiwa ghali kwa kaya nyingi," anaiambia TRT Afrika.

Alassane hupata mafiuta yanatumiwa kulainisha injini ya gari yaliyotumika gereji. Mwenye gereji huuza lita moja kwa 40 CFA franc (US $0.065).

"Kwa bei ya CFA 200, mtumiaji wa jiko la mafuta taka anaweza kuandaa angalau milo mitatu kila siku kwa mwezi mmoja," anasema.

Familia inayomuunga mkono

Babake Alassane, Sheikh Thiam, siku zote alijua kwamba mwanawe alikuwa na akili ya ubunifu ambayo ilihitaji kufuatiliwa.

Ingawa hakuweza kumudu masomo, Sheikh alimsajili Alassane katika taasisi ya mafunzo ya uchomeleaji vyuma.

Kijana huyo alisafiri hadi Touba, maili nyingi kutoka kwa wilaya yake, ili kuboresha ujuzi wake na kumrudisha mtu aliyebadilika.

Jiko la Alassane limefaidi wakazi wapatao 26,000 . /Picha: Alassane Thiam

Akiwa na ujuzi wa kuchomelea vymua, alianza kutengeza jiko ambalo lingemfanya kuwa maarufu huko Mbar na kwingineko.

"Kila mtu anavutiwa na jinsi mfumo wangu ulivyo rahisi na unaofanya kazi. Unawasha moto na kuzungusha kibomba cha kuwasha, basi, hivyo tu" Alassane anasema.

Mpango wake wa uuzaji ni wa kutumia mfumo wa zamani wa kujitangaza bila kutumia mitandao ya kijamii.

"Mashine ya mafuta" ya Alassane tayari inahitajiwa kwa wingi, na hivyo kumfanya aongeze uwezo wa uzalishaji na kubadilisha viwanda.

Sasa ameajiri wafanyakazi wa kumsaidia kutengeneza mashine nyingi zaidi na kufunga mfumo huo katika mashine za kilimo, matrekta na baiskeli za magurudumu matatu.

"Tunatoza bei zinazotuwezesha kufidia gharama zetu na, wakati huo huo, kusaidia kaya ambazo hazina uwezo mkubwa wa kununua. Tunauza jiko moja kwa franc 75,000 za CFA ($120) na jiko la burner mbili kwa mara mbili ya bei," anasema Alassane.Ukosefu wake wa digrii za masomo haumsumbui tena. Anapojitosa katika eneo jipya kwa kutengeneza milango ya chuma na bidhaa nyingine, Alassane anatamani kutoa ajira kwa watu wengi zaidi na kunufaisha jamii yake."Nina matumaini ya kuungwa mkono na serikali au washirika binafsi ili kuuza bidhaa zangu kwa kiwango kikubwa, hasa jiko langu la mafuta taka," anaiambia TRT Afrika.

TRT Afrika