Vita nchini Sudan vimesambaa kutoka Khartoum  / Photo: Reuters

Jeshi la Sudan siku ya Jumatano lilishutumu Vikosi vya Rapid support Forces (RSF) kwa "kumteka nyara na kumuua" gavana wa jimbo la Darfur Magharibi,

Hii inakuja huku mzozo wa madaraka kati ya majenerali wanaoongoza pande hizi mbili kuiingiza nchi hiyo katika vita vikali tangu tahere 15 Aprili mwaka huu.

Khamis Abdullah Abbakar aliuawa huko El Geneina, maafisa wa serikali wameliambia shirika la habari la Reuters.

Abbakar alikuwa ameishutumu RSF na wanamgambo washirika wa ghasia ambazo aliziita "mauaji ya halaiki."

Mauaji yake yalimaanisha kwamba RSF imeongeza "sura mpya kwenye rekodi yake ya uhalifu wa kinyama ambayo imekuwa ikifanya dhidi ya watu wote wa Sudan," jeshi lilisema kwenye mtandawo wake wa Facebook, likiliita tukio hilo "kitendo cha kikatili."

Mapambano ya madaraka

RSF haijatoa maoni yoyote kuhusu tuhuma hiyo.

Mapambano kati ya mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, anayejulikana kama Hemedti, yalisababisha mapigano tangu katikati ya Aprili.

Zaidi ya watu 1,800 wameuawa tangu mapigano yaanze, kulingana na Mradi wa Data wa (ACLED).

Mapigano yamewalazimu takriban watu milioni mbili kutoka makwao, wakiwemo 476,000 ambao wametafuta hifadhi katika nchi jirani, Umoja wa Mataifa unasema.

TRT Afrika na mashirika ya habari