Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, wamekutana na upinzani kutoka jeshi la DRC na washirika wake, vikiwemo vikosi kutoka Burundi, siku ya Ijumaa, kimesema chanzo kimoja kutoka DRC.
Kwa upande wake, Rwanda inaendelea kusisitiza kuwa haijatuma vikosi vyake ndani ya DRC, kama madai ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa yanavyosema.
Safari ya kuelekea Bukavu
Kikosi cha wapiganaji wapatao 1,500, wakiwemo wanamgambo kutoka Burundi wamepelekwa kuulinda mji wa Nyabibwe ambao unaelekea Bukavu, chanzo kimoja kimesema.
Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi umekuwa sio wa kuridhisha huku kitendo cha wanajeshi wa Burundi kuwasaidia wenzao wa DRC, kikitajwa kuhatarisha zaidi amani ya kanda, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa msemaji wa M23 Willy Nangaa, waasi hao wameendelea kupambana na vikosi kutoka Burundi, wakati vikijaribu kulinda miji ya Goma na maeneo mengine dhidi ya uvamizi.