Vita vinaendelea Sudan tangu tarehe 15 Aprili mwaka huu

Mwanadiplomasia mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, UN, ameilaumu kwa kiasi shirika hilo la kimataifa kwa kushindwa kuzuia mzozo nchini Sudan ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 550 na wengine 3,500 kujeruhiwa.

Jamal Benomar, ambaye alifanya kazi katika Umoja wa Mataifa kwa miaka 25, anasema Baraza la Usalama lilipaswa kuingilia kati ili kuzuia mzozo kati ya uongozi wa juu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Sudan, ASF, na Kikosi cha Rapid Support Forces, RSF.

Anasema kilichojiri Sudan anaweza kukilinganisha na wakati alipoonya Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen alipokuwa akifanya kazi.

"Jumuiya ya Kimataifa ilipaswa kuchukua hatua mapema sana. Nakumbuka tangu siku zangu katika Umoja wa Mataifa, nilipokuwa ninahudumia Yemen, nilisihi baraza la usalama mapema mwaka 2014 kuchukua hatua dhidi ya waharibifu [wa mabadiliko ya amani], lakini walisitasita sana," alisema Benomar.

"Nimeona ulegevu huo ukifanyika nchini Sudan, hata sasa. Baadhi ya wenye mamlaka wanasitasita kuweka shinikizo la kweli kwa pande zinazozozana,” aliongeza.

Jamal Benomar auliza wamewaangusha Sudan | Picha: Reuters

Kukiri kwa Guterres

Matamshi ya Benomar yanakuja siku chache baada ya Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), kusema mzozo unaoendelea nchini Sudan ulichukua shirika hili la kimataifa kwa "mshangao".

"Suala hili nchini Sudan limeshangaza Umoja wa Mataifa," Guterres alisema Jumatano katika ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. "Tulikuwa na matumaini kwamba mazungumzo yatafanikiwa.

Hatukutarajia hili kutokea,” aliongeza. Guterres aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa haujafaulu kujaribu kuzuia mzozo huo.

“Tulishindwa kulikwepa lisitokee. Sidhani kama kulikuwa na jambo lolote ambalo tulipaswa kufanya [ambalo hatukufanya] ili kulizuia [ lisitokee]. Tulikuwa na hakika kwamba hilo halingetokea.

” Majenerali wa Kikosi cha Wanajeshi wa Sudan (SAF) na Wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF) wanaendelea kuzozana juu ya udhibiti wa taifa hilo, na kukaidi makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo waliripotiwa kuingia mapema wiki hii.

Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huku mkanganyiko na wasiwasi ukiathiri juhudi za kuwahamisha, haswa katika mji mkuu Khartoum.

Juhudi za upatanishi Sudan

Benomar anasema suluhu la muda mrefu linaweza kufikiwa ikiwa wapatanishi katika vita wataunganisha juhudi zao.

“Kila mtu anafahamu kuwa kuna uchumi wa vita nchini Sudan, wanajua pia kwamba wananufaika na mitandao, ikiwemo miundombinu waliyoijenga. Nadhani Marekani na Umoja wa Ulaya wana ujuzi, ujuzi na taarifa zote zinazohitajika kuwabana waharibifu katika msingi wao wa kiuchumi.

Jamal Benomar, Mwanadiplomasia wa zamani wa Umoja wa Mataifa, UN

“Kuna haja ya kuwa na mpatanishi mmoja. Kumekuwa na nchi nyingi zinazohusika, kujaribu kupatanisha mgogoro huu - kutoka Saudi Arabia, Marekani, Kenya, na kisha kuna IGAD, Umoja wa Afrika na hivi karibuni tulisikia Israeli inataka kupatanisha mgogoro huu," aliiambia TRT Afrika.

"Tunachojua kutokana na uzoefu ni kwamba kuna haja ya kuwa na mpatanishi mmoja tu na wengine wote wakimuunga mkono mpatanishi mmoja pekee."

Benomar anasema juhudi za kurejesha amani zinaweza, hata hivyo, kutatizwa na mashirika yenye nguvu na nchi ambazo zina maslahi nchini Sudan.

“Kila mtu anafahamu kuwa kuna uchumi wa vita nchini Sudan, wanajua pia kwamba wananufaika na mitandao, ikiwemo miundombinu waliyoijenga. Nadhani Marekani na Umoja wa Ulaya wana ujuzi, ujuzi na taarifa zote zinazohitajika kuwabana waharibifu katika msingi wao wa kiuchumi.

Uanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Mjumbe huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa alipendekeza kuwa ni wakati muafaka kwa Afrika kupata uanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Kwa hakika Afrika inahitaji sauti katika Baraza la Usalama. Kumekuwa na mazungumzo kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama, lakini wale katika baraza wanataka kurefusha majadiliano haya. Hawataki madaraka yao yapunguzwe."

Siku ya Alhamisi, Umoja wa Mataifa ulitoa wito wa dola milioni 96 kusaidia watu wanaokimbia migogoro nchini Sudan.

Peter Van der Auweraert, mratibu wa misaada ya kibinadamu kwa muda wa Sudan Kusini, alisema zaidi ya watu 32,500 wamevuka hadi Sudan Kusini tangu kuzuka kwa vita Aprili 15.

TRT Afrika